Saturday 11 September 2010

CHEKI: www.sokainbonbo.com

Neville: ‘Naichukia zaidi Man City kupita Liverpool!’
Beki wa Manchester United, Gary Neville, ameiponda Manchester City na pia kudai kuwa, kwake yeye, Liverpool ni bora kupita Man City.
Msimu uliokwisha, Neville alizua mzozo pale alipomponda Carlos Tevez, Mchezaji aliewahi kuichezea Man United na kisha kuhamia Man City, na pia alipoenda kushangilia ushindi wa Man United mbele ya Mashabiki wa Man City waliokuwepo Old Trafford kuitazama mechi ya Man United v Man City.
Neville ametamka: “Nawaheshimu Liverpool kama Klabu yenye utamaduni mzuri na historia ndefu na si Klabu iliyoibuka hivi karibuni na kutumia mifedha kiwehu!”
Walcott nje Wiki 6
Winga wa Arsenal Theo Walcott atakuwa nje kwa Wiki 6 akiuguza enka yake aliyoumia akiichezea England dhidi ya Uswisi Jumanne iliyopita.
Habari hizi zimethibitishwa na Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema Walcott atakuwa nje Wiki 4 hadi 6.
Msimu huu Walcott ameanza kwa moto mkali na kufunga bao 4 katika mechi 4 alizochezea Arsenal.
Winga huyo atazikosa mechi dhidi ya Bolton, Sunderland, West Bromwich na mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Braga na Partizan Belgrade.
Rufaa ya Evra yatupwa!
Nahodha wa Ufaransa, Patrice Evra, ataendelea na kifungo chake cha mechi 5 alichopewa na FFF, Chama cha Soka Ufaransa, kwa kuongoza mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini Uafarnsa ilipokuwa kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Wachezaji wa Ufaransa waligomea mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa baada ya kugombana na Kocha Raymond Domenech.
Pamoja na Evra, Wachezaji wengine wa Ufaransa waliofungiwa kufuatia sakata hilo la Kombe la Dunia ni Anelka, mechi 18, Franck Ribery, mechi 3 na Jeremy Toulalan, mechi moja.
Evra alikata rufaa kupinga kifungo hicho kwa Kamati ya Rufaa ya FFF lakini kamati hiyo imesema adhabu itabaki pale pale.

No comments:

Powered By Blogger