Wednesday 8 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Wakaguzi wa FIFA wapo USA
Timu ya Wakaguzi wa FIFA ya Wagombea Uenyeji wa Kombe la Dunia ipo Marekani na tayari imeshatembelea New York, Ikulu ya Marekani huko Washington na inategemewa kupitia jumla ya Miji mingine mitatu katika ukaguzi wao wa Siku 3.
Wakaguzi hao sita wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Chile, Harold Mayne-Nicholls, pia watatembelea Miji ya Miami, Dallas na Houston.
Timuhiyo ya Wakaguzi tayari washapitia Nchi Waombaji 8 kati ya 9 na watamalizia ukaguzi wao huko Qatar kati ya Septemba 13 hadi 17.
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Marekani ya Kugombea Uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia.
Inategemewa Nchi ya Ulaya itapewa Uenyeji wa Fainali za 2018 na Wagombea ni England, Russia, Spain na Ureno kwa pamoja na Ubelgiji na Uholanzi kwa pamoja.
Fainali za Mwaka 2022 zinashindaniwa na USA, Australia, Japan, Korea Kusini na Qatar.
Uamuzi wa nani atapewa Uenyaji wa Fainali hizo za Kombe la Dunia utafanyika Desemba 2 na Kamati Kuu ya FIFA yenye Watu 24.
Fainali zijazo za Mwaka 2014 zitafanyika Nchini Brazil.

No comments:

Powered By Blogger