Thursday 23 September 2010

Wenger: ‘Ntaendelea Ukocha labda afya igome!’
• Adai Klabu Tajiri zinamkosesha Ubingwa!
WENGER ndani ya OLD TRAFFORD
Akiwa na umri wa Miaka 61 na tayari amesaini Mkataba mpya hadi Mwaka 2014, Arsene Wenger, ambae alitua Arsenal Septemba 1996, amesema ataendelea kuwa Kocha na kukuza vipaji vya Vijana hadi afya yake itakapogoma.
Wenger amebainisha kwamba bado yuko Arsenal kwa miaka mingi sasa si kwamba hatakiwi kwingine ila tu ni kwa sababu Arsenal imempa uhuru na haingiliwi chochote kwenye kazi yake.
Lakini amekiri kuwa siku moja atarudi kwao Ufaransa na ipo Klabu moja ambayo iko moyoni mwake na hiyo ni Strasbourg.
Kwa sasa, Wenger ana kibarua kikubwa cha kuifanya Arsenal ishinde Kombe lake la kwanza tangu 2005 waliponyakua FA Cup na pia kutwaa tena Ubingwa wa England tangu Msimu wa 2003/4 walipoutwaa Ubingwa bila kufungwa hata mechi moja.
Licha ya kutopata mafanikio yeyote kwa Miaka mitano, Wenger amejitetea: “Watu wanasema hatujashinda kitu kwa Miaka mitano sasa. Ni kweli, lakini siku zote tupo juu licha ya Klabu kuwa na matatizo. Arsenal wamejenga Uwanja mpya inabidi tulipe hilo, na tumejenga Kikosi kipya! Utasema nini ikiwa Manchester City iliyotumia Pauni Milioni 200 Msimu huu haishindi Kombe lolote?”
Wenger alisisitiza: “Sababu kubwa hatujashinda Kombe lolote kwa Miaka mitano ni kuwa tupo kwenye Ligi bora Duniani na tunacheza na Klabu tajiri!”

No comments:

Powered By Blogger