Thursday 23 September 2010

FERGIE: 'Kuchagua Mchezaji Bora Utata!'
Andersson, Giggs & Rooney
Alex Ferguson amekiri ni vigumu kwake kuchagua nani ni Mchezaji Bora wa Manchester United katika kipindi chake cha Miaka 24 Klabuni hapo.
Ferguson, alieanza utawala wake Man United Mwaka 1986, allikuwa akihojiwa na Stesheni ya TV CNN, na alikiri ugumu wa swali hilo ingawa aliwataja Wachezaji 7 kuwa ni wazuri.
FERGIE
Ferguson aliiambia CNN kuwa Bryan Robson aliekuwa Nahodha wake na pia wa England alikuwa kipenzi cha Wachezaji wenzake na pia makini kwenye mbinu.
Pia alimtaja Roy Keane kama kiongozi bora na ni mpiganaji.
Ferguson alisema: “Paul Scholes ni Mchezaji wa kushangaza, siku zote ataonekana kama Mchezaji bora katika historia ya Man United. Alikuwepo Cantona, pia Giggs na Ronaldo, Rooney na wote hawa ni Wachezaji mahiri na ni ngumu sana kusema nani bora!”
FIFA yaonya dili za kura za Uenyeji Kombe la Dunia
FIFA imezionya Nchi zinazogombea Uenyeji wa Kombe la Dunia kwa Mwaka 2018 na 2022 kuwa ni marufuku kuingia dili na Nchi nyingine ili wapigiwe kura.
Onyo hilo la FIFA limekuja baada ya kuibuka fununu kuwa kuna Nchi moja huko Ulaya inayogombea Uenyeji wa Mwaka 2018 imefikia makubaliano na nyingine inayogombea 2022 ili wapigiane kura kusaidiana.
Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema FIFA wana njia zao za kuchunguza mambo na kufuatilia nini kinafanywa na Wagombea Uenyeji wote.
Nchi za Ulaya zinazogombea Uenyeji wa Mwaka 2018 na 2022 ni England, Russia, Spain/Portugal, kwa pamoja, Netherlands/Belgium, kwa pamoja, na pia ipo USA inayowania nafasi hiyo.
Qatar, Australia, Japan na Korea Kusini zinagombea 2022 lakini ikiwa Nchi ya Ulaya itashinda Uenyeji wa 2018 Nchi nyingine za Ulaya zitaondolewa kwenye kinyang’anyiro cha 2022.
Kamati Kuu ya FIFA itatoa uamuzi wa nani watakuwa Wenyeji hapo Desemba 2.
Vela afungiwa Miezi 6
CARLOS VELA
Straika wa Mexico na pia Arsenal, Carlos Vela, pamoja na mwenzake Efrain Juárez wamefungiwa Miezi 6 na Chama cha Soka cha Mexico kwa kukiuka kanuni baada ya kuangusha bonge la Pati kwenye Hoteli iliyopiga kambi Timu ya Taifa ya Mexico mara baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Colombia Mwezi uliopita.
Wachezaji wengine wa Mexico 11 waliadhibiwa kwa kupigwa Faini ya Pauni 2500 kila mmoja na hao ni Giovani dos Santos, Javier Hernández, Guillermo Ochoa, Francisco Rodriguez, Carlos Salcido, Andrés Guardado, Gerardo Torrado, Pablo Barrera, Rafael Márquez, Enrique Esqueda na Héctor Moreno.

No comments:

Powered By Blogger