Sunday 19 September 2010

Chelsea 4 Blackpool 0
Mabingwa Watetezi Chelsea leo tena wameendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuifunga Blackpool mabao 4-0 Uwanjani Stamford Bridge huu ukiwa ushindi wao wa 5 mfululizo tangu Msimu mpya wa Ligi Kuu uanze na kuwafanya wabaki kileleni kwa pointi 4 mbele dhidi ya Arsenal na Man United zinazofungana pointi kwa kuwa na pointi 11.
Leo mabao yote ya Chelsea yalifungwa Kipindi cha Kwanza wafungaji wakiwa Kalou, Malouda, bao mbili, na Drogba.
Mechi inayofuata kwa Chelsea kwenye Ligi Kuu ni ile ya ugenini Jumamosi ijayo huko City of Manchester Stadium watakapokumbana na ‘Timu Tajiri’ Manchester City na safari hii mechi hii ikiwa tofauti kwa Mabingwa hao kwa kuonekana kidogo ngumu baada ya kuanza Ligi Kuu na kuziponda Timu ubwete kama vile West Bromwich Albion, Wigan Athletic, Stoke City, West Ham United na leo Blackpool.
Vikosi vilivyoanza:
Chelsea: Cech, Ferreira, Ivanovic, Alex, Cole, Essien, Mikel, Ramires, Kalou, Drogba, Malouda.
Akiba: Turnbull, Benayoun, Zhirkov, Sturridge, Anelka, Bruma, Kakuta.
Blackpool: Gilks, Eardley, Evatt, Baptiste, Keinan, Crainey, Grandin, Adam, Vaughan, Varney, Campbell.
Akiba: Halstead, Southern, Harewood, Ormerod, Taylor-Fletcher, Cathcart, Carney.
Refa: Mark Clattenburg
Wigan 0 Man City 2
Carlos Tevez na Yaya Toure leo wamewapa ushindi Manchester City walipofunga bao mbili katika mechi ya Ligi Kuu ambayo Man City walishinda 2-0 ugenini.
Ushindi huu umeiweka Man City nafasi ya 4 wakiwa na pointi 8 kwa mechi 5.
Juu yao wako, jirani zao Man United wenye pointi 11 sawa na Arsenal.
Chelsea ndie wanaongoza wakiwa na pointi 15 kwa kushinda mechi zao zote 5 za Ligi Kuu.
Vikosi vilivyoanza:
Wigan: Al Habsi, Boyce, Gohouri, Alcaraz, Figueroa, N'Zogbia, Thomas, McCarthy, Diame, Rodallega, Di Santo.
Akiba: Kirkland, Watson, Boselli, Moses, Steven Caldwell, Gomez, Stam.
Man City: Hart, Richards, Kompany, Toure, Zabaleta, De Jong, Toure Yaya, Barry, Silva, Milner, Tevez.
Akiba: Given, Wright-Phillips, Adam Johnson, Santa Cruz, Vieira, Jo, Boyata.
Refa: Lee Probert

No comments:

Powered By Blogger