• Kuyt kurejea mapema baada ya kupona!
Beki wa Liverpool Daniel Agger amezikana taarifa kuwa alimpinga Meneja wake Roy Hodgson kuhusu mbinu anazotumia ambazo huwataka Mabeki kutotuliza mipira nyuma na kupiga mbele ndefu haraka.
Habari za kumpinga Hodgson ziliibuka Nchini kwa Agger huko Denmark lakini Beki huyo wa Kimataifa mwenye Miaka 25 amezikana na kusema si za kwake.
Ilidaiwa kuwa Agger alisema yeye ni Mchezaji aliezoea kutuliza mpira chini na kuanza kwa pasi na si kuosha mipira kwa kubutua mipira mirefu mbele kama wanavyolazimishwa na Meneja wao Hodgson.
Wakati huo huo, Liverpool wamepata habari za faraja kubwa kwao baada ya Fowadi wao mpiganaji mkubwa uwanjani Dirk Kuyt kuanza tena mazoezi baada ya kuumia bega akiwa na Timu ya Taifa ya Uholanzi.
Kuyt amekuwa nje ya uwanja kwa Wiki mbili sasa na ilihofiwa atakuwa nje kwa muda mrefu uliokadiriwa kuwa hadi Wiki 5.
Hodgson amesema Kuyt huenda akacheza Wikiendi hii kwenye mechi na Sunderland ya Ligi Kuu au ile inayofuata ya EUROPA LIGI Wiki ijayo huko Uholanzi dhidi ya Klabu ya zamani ya Kuyt Utrecht.
Bebe kuwemo Kikosi cha Man United Carling Cup
Bebe, Chicharito, Sir Alex na Smalling |
Bebe, Miaka 20, amehamia Man United kutoka Vitoria Guimaraes ya Ureno lakini tangu atue hapo hajacheza mechi yeyote ya Kikosi cha Kwanza mbali ya kucheza mechi moja tu ya Kikosi cha Rizevu.
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amethibitisha Kikosi kitakachocheza kesho kitakuwa mchanganyiko wa Chipukizi na wale wazoefu.
Ferguson amesema: “Tuna Wachezaji wengi na wengi wanahitaji mechi. Bebe na Macheda kesho watashiriki.”
Mwenyewe Bebe, akijibu tuhuma za baadhi ya Magazeti kuwa hastahili kuwemo Man United, ameomba Wadau kuwa wavumilivu na wataona cheche zake.
Bebe ametamka: “Nitakuwa moto kwa Man United. Lazima niwe fiti kwani soka la England ni tofauti. Sir Alex amesema anaridhishwa na mimi lakini nifanye mazoezi zaidi.”
Bebe pia ametoa shukran zake kwa Wachezaji wenzake kwa kumsaidia kuizoea Man United hasa Mapacha, Rafael na Fabio, Nani na Anderson kwa vile wanaongea nae Kireno.
No comments:
Post a Comment