Tuesday 21 September 2010

Wenger akiri makosa, apigwa Faini na Kifungo mechi 1
Arsene Wenger amekubali makosa yake aliyoshitakiwa na FA baada ya kumvaa Refa wa Akiba Siku ya Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu mara baada ya Sunderland kusawazisha bao dakika za majeruhi na Wenger kulalamikia muda umekwisha.
Kufuatia kukiri makosa hayo, Wenger sasa atalipa Faini ya Pauni 8,000 na kuikosa mechi ya leo ya Carling Cup ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Tottenham huko White Hart Lane.
Kwa kukiri haraka kosa lake, Wenger amepata ile adhabu ya kawaida ambayo hupewa kila Mtu anaekiri mara baada ya kushitakiwa na hivyo kukwepa kesi kwenda kwenye Kamisheni Huru ya Sheria ambayo isingekaa haraka na kungekuwapo uwezekano wa Wenger kuadhibiwa na kuikosa BIGI MECHI hapo Oktoba 3 huko Stamford Bridge ambako Arsenal wataenda kuivaa Chelsea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Wenger kufungiwa mechi tangu ahamie Arsenal Mwaka 1996 ingawa 2001alifungiwa Mechi 12 baada ya kumvaa Refa Msaidizi walipofungwa na Sunderland lakini adhabu hiyo ilifutwa baada ya kukata rufaa.

No comments:

Powered By Blogger