LIGI KUU: Leo siku ya Vigogo kutunguliwa!!
• Baada ya kuchapwa Chelsea nao Ze Gunners, Spurs chaliii!!!
• Liverpool chupuchupu!!!
Baada ya Chelsea kuchapwa 1-0 na Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema vikafuata vipigo kwa Vigogo wengine pale Arsenal walipopigwa 3-2 wakiwa nyumbani Emirates na West Bromwich na pia Tottenham kutunguliwa 1-0 huko Upton Park na West Ham.
Bao lililowapa ushindi West Ham dhidi ya Tottenham lilifungwa kwa kichwa na Frederic Piquionne kwenye dakika ya 29.
Nao Liverpool, wakiwa nyumbani Anfield, walitoka sare 2-2 na Sunderland lakini wageni hao watakuwa na kila sababu ya kulalamika bao la kwanza la Liverpool kwani lilifungwa katika utata mkubwa.
Sunderland walipewa frikiki na wakati kila mtu alijua Michael Turner alikuwa akimsogezea Kipa wake ili aipige frikiki hiyo Fernando Torres akaunasa mpira huo na kumpasia Kuyt aliefunga.
Darren Bent aliisawazishia Sunderland kwa penati na pia kufunga tena bao la pili lakini Steven Gerrard akarudisha bao na kuiokoa Liverpool toka kwenye kipigo.
Huko Emirates ndipo kulikuwa na kindumbwendumbwe baada ya wenyeji Arsenal kuendeshwa mchakamchaka kipindi cha pili na West Bromwich Albion kufuatia mechi kuwa 0-0 hadi mapumziko ingawa mambo yangekuwa mabaya kwa Arsenal laiti kama West Brom wangefunga penati kipindi hicho cha kwanza ambayo ilipigwa na Chris Brunt na Kipa Almunia kuiokoa.
Mnigeria Peter Odemwingie ndie alieipatia West Brom bao la kwanza, Gonzalo Jara akapiga la pili na Jerome Thomas akaunga bao la 3 kuwafanya West Brom wawe mbele 3-0.
Samir Nasri akafufua matumaini ya Arsenal alipopachika bao mbili na kufanya magoli yawe 3-2 lakini West Brom walisimama imara na kupata ushindi wao mnono wa pili kwa Wiki hii ambapo Jumatano waliifunga Manchester City 2-1 kwenye Carling Cup.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Almunia, Sagna, Squillaci, Koscielny, Clichy, Song, Diaby, Eboue, Nasri, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Rosicky, Vela, Denilson, Wilshere, Djourou, Emmanuel-Thomas.
West Brom: Carson, Jara, Pablo, Olsson, Shorey, Mulumbu, Scharner, Brunt, Morrison, Thomas, Odemwingie.
Akiba: Myhill, Tchoyi, Reid, Dorrans, Zuiverloon, Fortune, Cox.
Refa: Michael Oliver
LIGI KUU ENGLAND:
MATOKEO:
Jumamosi, 25 Septemba 2010
Man City 1 Chelsea 0
Arsenal 2 West Brom 3
Birmingham 0 Wigan 0
Blackpool 1 Blackburn 2
Fulham 0 Everton 0
Liverpool 2 Sunderland 2
West Ham 1 Tottenham 0
RATIBA:
Jumapili, 26 Septemba 2010
[saa 8 mchana]
Bolton v Man Utd
[saa 10 dak 5 jioni]
Wolverhampton v Aston Villa
[saa 12 dak 10]
Newcastle v Stoke
No comments:
Post a Comment