Friday 24 September 2010

Fergie: ‘Rooney ameelemewa!’
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri Wayne Rooney anaandamwa mno na Vyombo vya Habari na hilo limearhiri uchezaji wake.
Hivi karibuni Rooney alilipuliwa Magazetini kuwa alitembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
Msimu huu, Rooney amefunga bao moja tu kwa Timu yake na Ferguson hakumpanga kwenye mechi ya huko Goodison Park dhidi ya Tinu ya Rooney ya zamani Everton akihofia kusakamwa na Mashabiki.
Ferguson amesema Rooney amekuwa kwenye presha na hilo limemchosha akili.
Wakati huo huo, Ferguson amedai ratiba ya Msimu huu imeibeba Chelsea kwa kuanza na Timu ubwete.
Ferguson ametamka: “Wameanza vizuri mno. Pengine ratiba hiyo wameipanga wenyewe. Msimu uliokwisha walimaliza ratiba yao kwa kucheza na Timu dhaifu na kuzifunga lundo ya magoli na Msimu huu wameendelea hivyo hivyo!”
Arsenal yapata Faida
Klabu ya Arsenal imetangaza kuwa imepata faida ya Pauni Milioni 56 kwa Mwaka wa Fedha uliomalizika Mei 2010 na faida hiyo ina ongezeko la Pauni Milioni 10.5 toka ya Mwaka uliopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema deni la Klabu hiyo limeshuka kutoka Pauni Milioni 297.7 hadi 135.6 kwa sababu waliuza Fleti zao 362 zilizokuwa Uwanja wao wa zamani wa Highbury na kulipa deni.

No comments:

Powered By Blogger