Monday 20 September 2010

Wenger afunguliwa mashitaka na FA
Arsene Wenger amefunguliwa mashitaka na FA kwa kutumia lugha chafu na utovu wa nidhamu kufuatia vitendo vyake kwa Marefa wa mechi ya Ligi Kuu Jumamosi iliyopita walipotoka sare 1-1 na Sunderland.
Wenger alionekana akimvaa Refa wa Akiba Martin Atkinson mara baada ya Darren Bent wa Sunderland kufunga goli la kusawazisha dakika za majeruhi.
Lakini, Wenger baadae alikana kumsakama Atkinson na kusema: “Sikulalamika kwa Mtu. Katika zile dakika 4 za nyongeza kulikuwa hamna kitu cha kufanya muda uongezwe zaidi ya hapo. Lakini najua Refa anaweza kuongeza muda zaidi ya dakika 4.”
Kufuatana na kanuni mpya za FA za kuharakisha kesi, Wenger amepewa hadi Alhamisi ili kujibu mashitaka hayo na atapewa Faini ya Pauni 8,000 na kufungiwa mechi moja ikiwa atakubali makosa lakini akikana shauri lake litapelekwa kwa Kamati ya Sheria ambayo inaweza ikatoa adhabu kali zaidi.
Mancini kumruhusu Given kung’oka
Bosi wa Manchester City Roberto Mancini amesema atamruhusu Kipa Shay Given kuhama Dirisha la uhamisho likifunguliwa Mwezi Januari Mwakani.
Given amepoteza nafasi yake kama Kipa nambari wani na imechukuliwa na Joe Hart ambae ndie amedaka mechi zote 8 za Man City Msimu huu.
Mancini amesema: “Nimemwambia anaweza kubaki lakini naheshimu amuse wake akiamua kuondoka.”
Shay Given ameshatamka hawezi kubaki Man City ikiwa hatapangwa.

No comments:

Powered By Blogger