Saturday, 18 October 2008

Boro 0 Chelsea 5

Middlesbrough wakiwa nyumbani Uwanja wa Riverside wamecheza mpira mbovu wa chini ya kiwango na kuwafanya wanaoongoza LIGI KUU Chelsea kupata pointi 3 za chee na magoli matano bila ya hata kuonyesha kiwango chochote cha juu.
Ni mechi ambayo inapingana na imani ya wengi kuwa LIGI KUU UINGEREZA ndio bora duniani.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa 1-0 kwa bao lililofungwa na Kalou.
Baada ya mapumziko Juliano Belletti wa Chelsea akapachika bao la pili kwa mkwaju mkali. Bao la tatu lilimbabatiza beki wa Boro David Wheater baada ya shuti la Kalou.
Ni Kalou tena aliepiga krosi iliyomaliziwa na Frank Lampard kwa kichwa kufanya 4-0.
Karamu ya magoli ilimaliziwa na Florent Malouda baada ya Kipa wa Boro Ross Turnbull kutema shuti la Anelka.

Middlesbrough: Turnbull, Grounds, Wheater, Riggott, Taylor, Aliadiere, Shawky, O'Neil, Adam Johnson, Downing, Mido. AKIBA: Jones, Digard, Emnes, Alves, Bennett, John Johnson, Walker.
Chelsea: Cudicini, Bosingwa, Terry, Alex, Bridge, Belletti, Lampard, Mikel, Kalou, Anelka, Malouda. AKIBA: Hilario, Ivanovic, Sinclair, Ferreira, Deco, Mancienne, Stoch.

No comments:

Powered By Blogger