Tuesday 14 October 2008

INJINI YA MANCHESTER UNITED KUANZA KUNGURUMA TENA: Hargreaves na Carrick kuonekana uwanjani wikiendi hii!!

Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amethibitisha kwamba Wachezaji wake wawili ambao ndio injini ya Klabu yake, Michael Carrick na Owen Hargreaves sasa wamepona na watashuka tena uwanjani wikiendi hii wakati Mabingwa hao wa LIGI KUU watakapowakaribisha West Bromwich Old Trafford kwenye mechi ya LIGI KUU UINGEREZA siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba 2008. Baada ya Kiungo mwingine mahiri, Paul Scholes, kuumia na inaaminika atakuwa nje ya uwanja hadi Desemba, Man U walikuwa na uhaba mkubwa wa viungo na taarifa za kupona kwa Hargreaves na Carrick ni habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo.
Carrick ameshakosa mechi 6 tangu avunjike mfupa mguuni kwenye mechi waliyocheza Anfield na Liverpool mwezi Septemba na Hrgreaves ana tatizo la muda mrefu la goti ambalo hutulia na kurudi tena tangu ajiunge na Man U akitokea Bayern Munich mwezi Agosti mwaka jana.
Sir Alex Ferguson amesema Wachezaji wote wako kwenye mazoezi kamili na bila shaka watakuwemo kwenye kikosi cha mechi ya Jumamosi watakapocheza na West Bromwich.

No comments:

Powered By Blogger