Friday 17 October 2008

RIO: 'Kiwango cha Rooney kimepanda kwa sababu ya kutua Berbatov Man U!'

Rio Ferdinand, beki mahiri wa Mabingwa Manchester United, ambae pia alikuwa Nahodha wa England kwenye mechi mbili za England za kuwania kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010 ambazo zote walishinda dhidi ya Kazakhstan kwa mabao 5-1 na Belarus bao 3-1, amesema anaamini kuibuka upya kwa kiwango cha juu kwa Wayne Rooney kinatokana na Manchester United kumununua Dimitar Berbatov.
Katika mechi tatu zilizopita za England, Wayne Rooney amefunga mabao 5 baada ya kuichezea England kwa mwaka mmoja bila ya kufunga bao lolote.
Rio anasema: 'Nadhani Berbatov ametusaidia na amemsaidia Rooney kuinua kiwango chake. Kila mchezaji daima hutaka kumuonyesha mchezaji mpya ubora wake. Sasa huu ushindani uliopo Man U unazaa matunda.!'
Rio aliongeza: 'Rooney ni mchezaji hodari na ni jinamizi kwa beki yeyote anaepambana nae. Ni mpiganaji na daima huhangaika kutafuta ushindi kwa timu yake na hata mazoezini yuko hivyohivyo-ni mshindani mahiri!'
Nae Muargentina Carlos Tevez amekanusha vikali taarifa zilizogaa na zilizomnukuu yeye akitamka kuwa kiwango chake msimu huu kimeshuka kwani Klabu ya Manchester United inamchezesha tofauti na alivyozoea na hivyo kusababisha kuwa butu msimu huu kwani mpaka sasa amefunga goli moja tu.
Carlos Tevez amezikana taarifa hizo kwa kutamka: 'Sijafanya mahojiano na Mwandishi yeyote na kwa kweli nina furaha kuwa Manchester United. Mie nikiwa uwanjani nataka timu ishinde tu na sijali nacheza wapi na vipi.'

No comments:

Powered By Blogger