Friday, 17 October 2008

LIGI KUU: DONDOO ZA MECHI ZA VIGOGO ZA JUMAMOSI

Arsenal v Everton [Emirates Stadium, London, saa 11 jioni]

Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani huenda wakawakosa nyota wao William Gallas, Bacary Sagna na Nicklas Bendtner ambao wamerudi klabuni majeruhi baada ya kutoka kwenye Timu zao za Taifa zilizoshiriki michuano ya kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Arsenal ambao wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 13 wameshapoteza mechi mbili kwenye LIGI KUU msimu huu wakati msimu mzima uliopita walipoteza mechi 3 tu!
Tangu wahamie hapo Emirates Stadium wamepoteza mechi 2 za LIGI KUU ya kwanza ikiwa dhidi ya West Ham Agosti 2006 na ile ya juzi tu Septemba 27 walipofungwa na timu mpya LIGI KUU Hull City.
Everton wanashikilia nafasi ya 15 na wana pointi 8 ingawa hawajafungwa hata mechi moja ugenini tangu ligi ianze.
Refa kwenye mechi hii ni Peter Walton.

Liverpool v Wigan [Anfield, Liverpool saa 11 jioni]

Nyota na mfungaji wa Liverpool Fernando Torres ataikosa mechi baada ya kuumizwa kwenye mechi ya Nchi yake Spain ilipoifunga Belgium 2-1 kwenye KOMBE LA DUNIA.
Wigan hawajawahi kuwafunga vigogo wa LIGI KUU ingawa msimu uliopita kwenye mechi kama hii walitoka sare ya 1-1 baada ya Emile Heskey kuisawazishia dakika ya mwisho ya mchezo.
Refa: Alan Wiley

Middlesbrough v Chelsea [Riverside Stadium, saa 8 dak 45 mchana]

Chelsea ambao wanaongoza LIGI KUU watakuwa wanatetea rekodi yao ya kutofungwa mechi hata moja ya ligi tangu Mbrazil Luis Felipe Scolari ashuke Chelsea.
Middlesbrough ambao walianza ligi vizuri mwezi Agosti kwa kushinda mechi 4 lakini wakapoteza mechi zote walizocheza Septemba ingawa mwezi huu Oktoba wameanza kwa ushindi baada ya kuwafunga Wigan.
Refa: Phil Dowd

Manchester United v West Brom [Old Trafford saa 1 na nusu usiku]

Mabingwa watetezi Man U wataingia uwanjani kucheza na West Brom ambayo haijawahi hata siku moja kuifunga Man U kwenye historia ya LIGI KUU.
Refa: Mark Halsey

No comments:

Powered By Blogger