Tuesday 14 October 2008

ENGLAND: Nahodha John Terry na Ashley Cole kukosa mechi ya Jumatano na Belarus!

Nahodha wa Timu ya Taifa John Terry na Mlinzi Ashley Cole hawatacheza mechi ya Jumatano huko Minsk, Belarus dhidi ya Belarus katika mitoano ya kutafuta timu zitazocheza FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010 kwa kuwa wote ni majeruhi.
John Terry aliikosa mechi ya Jumamosi England walipoifunga Kazhakstan mabao 5-1 kwenye Uwanja wao wa Wembley katika mechi ya Kombe la Dunia.
Ashley Cole alicheza mechi hiyo ingawa alipata wakati mgumu sana pale alipozomewa na mashabiki wa England kwa kufanya kosa kubwa lililowazawadia Kazakhstan bao lao moja. Kitendo hicho cha kumzomea Cole kimelaumiwa vikali na wachezaji wa England.

MAREKANI KUSINI: Venezuela 0 Brazil 4; Ecuador 1 Chile o

Katika Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini la KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010, Brazil ilipata ushindi mnono ugenini Venezuela pale waliposhinda mabao 4-0 huku nyota wao Kaka akicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka jana na kufunga bao moja.
Mabao mengine ya Brazil yalifungwa na Robinho aliefunga bao 2 na Adriano 1.
Brazil wako nafasi ya pili katika Kundi hili linaloongozwa na Paraguay. Argentina ni wa tatu.

Nao Ecuador waliwafunga Chile 1-0 katika mechi ambayo Wachezaji watatu walipewa kadi nyekundu, wawili wa Ecuador na mmoja wa Chile

No comments:

Powered By Blogger