Chama cha Soka Ulaya, UEFA, kimesimamisha kwa muda ile adhabu ya kuufungia Uwanja wa Atletico Madrid ya Spain, Vicente Calderon Stadium, mjini Madrid, ya kutochezewa mechi 3 kwa sababu ya vurugu za Mashabiki wa Klabu hiyo zilizoambatana na vituko vya ubaguzi wa rangi walizofanyiwa Marseille ya Ufaransa kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwanzoni mwa mwezi huu.
Hatua hii ya kusimamisha adhabu hii kwa muda kufuatia rufaa ya Atletico Madrid inamaanisha mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya Jumatano ijayo tarehe 22 Oktoba 2008 itachezewa hapohapo Uwanja wa Vicente Calderon.
Mbali ya Atletico Madrid kukata rufaa, Liverpool nao walilalamika kuwa adhabu hiyo ya kuufungia uwanja huo pia inawaadhibu Mashabiki wao na kuwatia hasara kwani walishafanya mipango siku nyingi kwenda mjini Madrid kuishangilia Liverpool na hivyo kufanya mechi kuchezwa nje ya Madrid ni usumbufu na hasara kwao.
No comments:
Post a Comment