Tuesday 14 October 2008

KOMBE LA DUNIA: BELARUS v ENGLAND= Nani kucheza kiungo?
GERRARD AU LAMPARD?

Mjadala, mabishano, malumbano na sasa yamefika kwa Meneja wa England, Fabio Capello, na hata wahusika wenyewe wakuu- Steven Gerrard na Frank Lampard.
Uingereza nzima kuanzia kwa Washabiki, Waandishi, Wataalam wa Soka na hata Meneja wa England sasa wamekumbwa kwenye utata wa je Steven Gerrard na Frank Lampard wanaweza kucheza timu moja?
Wengi, hasa Waandishi na Wataalam wa Soka, wametoa takwimu na vithibitisho kadhaa vya mechi walizocheza pamoja wakiwa Timu ya Taifa ya England na kila kitu kimethibitisha kwamba nyota hao wawili wanaotamba kwenye Klabu zao za Chelsea na Liverpool hawawezi kucheza timu moja kwa wakati mmoja.
Waliobobea kwenye soka wanadai wote wawili wanacheza staili ya aina moja na kwa mfumo unaotumiwa na England haiwezekani wakacheza pamoja.
Lakini, Meneja wa England, Fabio Capello amedai: 'Hivi watu kwa nini wanauliza kuhusu Gerrard na Lampard? Nasema wanaweza kucheza pamoja! Ni mastaa, wachezaji mahiri hawa!'
Kitu cha kushangaza ni kuwa mwenyewe Steven Gerrard ambae ni Nahodha wa Liverpool amekiri: 'Ntakuwa mkweli sijawahi kuichezea England vizuri kama nnavyoichezea Liverpool. Nadhani tatizo langu ni kwamba nataka kufanya kila kitu peke yangu uwanjani, kuzunguka uwanja mzima kama vile hakuna wengine wanaoweza kuiendesha timu! Hili Capello ameligundua na tumeongea na hata Meneja wa Liverpool Rafael Benitez ametaka nitulize boli.'
Gerrard anaendelea kukiri hata akiachwa mechi ya kesho hasikitiki kwani kwake ushindi kwa England ndio kitu muhimu zaidi.

No comments:

Powered By Blogger