Friday, 17 October 2008

BAADA YA KIPIGO CHA CHILE, MENEJA WA ARGENTINA AMWAGA UNGA!!!!!

Meneja wa Timu ya Taifa ya Argentina, Alfio Basile, amejiuzulu wadhifa wake huo mara baada ya Argentina kupigwa bao 1-0 na Chile katika mechi ya Kundi la Nchi za Marekani Kusini la kuwania kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Rais wa Chama cha Soka cha Argentina, Julio Grondona, amesema licha ya kumbembeleza Basile asijiuzulu Kocha huyo aligoma.
Alfio Basile ashawahi kuwa Meneja wa Argentina katika kipindi cha nyuma kati ya mwaka 1990 hadi 1994.
Katika Kundi la Nchi hizo za Marekani ya Kusini, Argentina inashikilia nafasi ya 3 ikiwa nyuma ya Paraguay inayoongoza na Brazil ni ya pili. Timu nne za juu za Kundi hili ndizo zinaingia FAINALI KOMBE LA DUNIA moja kwa moja.
Inasemekana nafasi ya Alfio Basile huenda ikachukuliwa na mmoja kati ya Kocha wa Timu ya Vijana wa Argentina Sergio Batista au Kocha wa Klabu ya River Plate Diego Simeone ama Miguel Angel Russo.

No comments:

Powered By Blogger