Saturday 21 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Arsenal 6 Blackpool 0
• Walcott ameremeta kwa bao 3!!!
Arsenal wakiwa kwao Emirates leo wametoa somo kwa Timu mpya Blackpool ambayo wiki iliyokwisha iliitandika Wigan bao 4-0 kwa kuibugiza mabao 6-0 huku bao 3 zikifungwa na Winga Theo Walcott ambae leo aling’ara sana.
Blackpool waliijikuta maji shingoni baada ya dakika 32 tu, huku wakiwa nyuma kwa bao 1 la Walcott la dakika ya 13, wakajikuta wakitoa penalti pamoja na Kadi Nyekundu kwa Beki wao Ivan Evatt aliemwangusha Marouane Chamakh ndani ya boksi.
Penalti hiyo ilifungwa na Andre Arshavin.
Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Walcott, dakika ya 39 na 58, Abou Diaby, dakika ya 49 na Marouane Chamakh dakika ya 83.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Almunia, Sagna, Song, Vermaelen, Clichy, Diaby, Wilshere, Walcott, Rosicky, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Fabregas, van Persie, Vela, Djourou, Eboue, Gibbs.
Blackpool: Gilks, Baptiste, Evatt, Cathcart, Crainey, Sylvestre, Vaughan, Adam, Grandin, Harewood, Taylor-Fletcher.
Akiba: Halstead, Eardley, Ormerod, Basham, Edwards, Demontagnac, Keinan.
Refa: Michael Jones
KWA UFUPI: Mechi nyingine za Ligi Kuu
Everton 1 Wolverhampton 1
Ingawa walitawala mechi hii na pia wakiwa nyumbani, Everton walijikuta wakitoka sare 1-1 na Wolves waliojitutumua sana.
Everton ndio walipata bao mwanzo kupitia Tim Cahill dakika ya 43 lakini Wolves walisawazisha dakika ya 74 kwa bao la Sylvan Ebanks-Blake.
West Ham 1 Bolton 3
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa West Ham baada ya Wiki iliyopita kuchapwa 3-0 na Aston Villa ugenini.
Leo wakiwa nyumbani wamepigwa 3-1 na pia kukosa penalti hafifu iliyopigwa na Carlton Cole na Kipa wa Bolton Jussi Jaaskelainen kuicheza.
Mabao ya Bolton yalifungwa na John Elmander, dakika ya 68 na 84, na jingine, la kwanza, West Ham walijifunga wenyewe kwa Beki Mathew Upson kupachika wavuni kwake.
Bao la west Ham lilifungwa na Mark Noble kwa penalty dakika ya 79.
Birmigham 2 Blackburn 1
Blackburn walitangulia kupata bao dakika ya 54 Mfungaji akiwa Steve Nzonzi lakini Birmingham wakazinduka na kufunga bao mbili dakika ya 57 na 71, Mfungaji wa yote akiwa ni Craig Gardner.
Stoke City 1 Tottenham 2
Mabao mawili ya Gareth Bale, dakika ya 20 na 30, yamewapa Tottenham ushindi wa 2-1 ugenini.
Boa la Stoke lilifungwa na Ricardo Fuller dakika ya 25.
West Brom 1 Sunderland 0
Wakiwa wametoka kwenye kichapo cha 6-0 huko Stamford Bridge Wiki iliyopita mikononi mwa Mabingwa Chelsea, WBA leo wamezinduka wakiwa kwao na kuitungua Sunderland bao 1-0 Mfungaji akiwa Mchezaji mpya Mnigeria Peter Odimwingie aliefunga dakika ya 81.

No comments:

Powered By Blogger