Tuesday 17 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United yaanua rasmi Vifaa Vitatu
Sir Alex Ferguson leo amewatambulisha rasmi Wachezaji watatu wapya huku akiwashambulia Wapinzani wao kwao kujiingiza kwenye matumizi ya ‘kamikaze’ katika kununua Wachezaji wapya kwa bei mbaya.
‘Kamikaze’ ni staili ya kujitoa muhanga waliotumia Askari wa Japan kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Ferguson hakuitaja Klabu yeyote kwa jina ambayo inatumia ‘kamikaze’ lakini, bila shaka, ni jirani zao Manchester City ambao tayari washatumia zaidi ya Pauni Milioni 125 kununua Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu huu mpya wakiwa pamoja na Mario Balotelli, ambae ndio kwanza amesaini, na James Milner, anaetegemewa kukamilisha uhamisho wake hapo kesho.
Ferguson alipiga picha ya pamoja na Wachezaji hao wapya Javier Hernandez aka Chicharito, Chris Smalling na Bebe.
Wakati wa utambulisho, Fergie alizungumza: “Katika Miaka mitatu au miwili iliyopita, tumeona Matajiri wakinunua Klabu na kufanya matumizi ya ‘kamikaze’. Inashangaza! Sioni kama kasi hiyo itapungua. Itachukua Miaka miwili au mitatu ndipo watagundua huwezi ukafanikiwa kwa matumizi kama hayo!”
Ferguson akasisitiza msimamo wa Man United kuendeleza Vijana: “Ukiwatunza vizuri, Vijana wanaendelea. Tena wanakuwa watiifu na waaminifu kwa Klabu kwa kuwa wanataka kulipa fadhila za malezi mazuri.”

No comments:

Powered By Blogger