Monday 16 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Bellamy apigwa marufuku Man City!!!
Straika wa Manchester City, Craig Bellamy, amepigwa marufuku asikanyage mazoezini mwa Manchester City hadi atakapotafutiwa mahala pa kwenda kufuatia amri aliyotoa Meneja wao Roberto Mancini.
Bellamy amekuwa na bifu la muda mrefu na Mancini na siku za hivi karibuni limelipuka baada ya jina lake kutokuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 25 waliosajiliwa na Klabu hiyo kwa ajili ya michuano ya EUROPA LIGI.
Bellamy alitamka wazi kuwa hawezi kubaki hapo ikiwa hatakuwemo kwenye Kikosi hicho na inaelekea jina lake limekatwa dakika za mwisho ili kuliongeza jina la Robinho anaelazimika kurudi Klabuni hapo baada ya Mkataba wake wa mkopo huko Santos kumalizika na Man City kugoma kumwongezea.
Inadaiwa kuwa Bellamy alipandwa na hasira na kuzirushia kwa Meneja na Wachezaji wenzake kadhaa na ndipo alipozuiwa kufanya mazoezi na Timu ya Kwanza na kupelekwa kucheza na Timu ya Rezevu lakini akaendeleza hasira zake.
Bellamy tayari amerudi kwao Wales na anategemewa kufanya mazoezi na Klabu ya nyumbani kwao Jijini Cardiff, Timu ya Cardiff City, ambayo pia imeonyesha nia ya kumchukua kwa mkopo Mchezaji huyo machachari lakini inaelekea wanashindana bei na Man City.
Awali Tottenham ilionyesha nia ya kumnunua Bellamy lakini Man City imegoma kwa vile wanaichukulia Timu hiyo kama mpinzani wao kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi za kucheza Ulaya.

No comments:

Powered By Blogger