Wednesday 18 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Anelka acheka kufungiwa
Nicolas Anelka, ambae jana alifungiwa mechi 18 na FFF, Chama cha Soka Ufaransa, amekidhihaki kifungo hicho na kuuita ni upuuzi na kichekesho.
Kamati ya Nidhamu ya FFF hapo jana iliamua kuwapa adhabu Wachezaji wanne kati ya watano waliofikishwa mbele yao kujibu tuhuma za kuongoza mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini kufuatia kufukuzwa kwa Nicolas Anelka baada ya kugombana na Kocha Raymond Domenech.
Anelka alipewa kifungo cha mechi 18 kutoichezea France na Evra amefungiwa mechi 5.
Ribery amepewa adhabu ya mechi 3 na Jeremy Toulalan mechi moja.
Eric Abidal amenusurika adhabu.
France haikushinda hata mechi moja huko Afrika Kusini na ilimaliza Kundi lake ikiwa mkiani na Timu nzima iligoma kufanya mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa kufuatia kugombana na aliekuwa Kocha wao Raymond Domenech.
Wachezaji wote 23 walisimamishwa kucheza mechi ya kirafiki na Norway iliyochezwa Oslo Agosti 11 na France kufungwa na Norway 2-1 na hatua hiyo ilipendekewa na Kocha mpya Laurent Blanc.
Anelka amesema: ‘Hawa watu ni wachekeshaji. Nakufa kwa kicheko! Upuuzi huo haunihusu kwa vile nilishtaafu Soka ya Kimataifa tangu Juni 19 siku niliyoondolewa Timu ya Ufaransa.”
Nasri kuwa nje Mwezi mzima
Samir Nasri atafanyiwa upasuaji wa goti lake na ataluwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mzima.
Nasri aliumia juzi kwenye mechi ya huko Anfield ya Ligi Kuu ambayo Timu yake Arsenal ilitoka sare 1-1 na Liverpool.
Kiungo huyo mwenye Miaka 23 alimaliza dakika 90 za mechi hiyo ya juzi lakini Klabu yake imethibitisha ni lazima afanyiwe operesheni ndogo.
Jumamosi Arsenal ipo nyumbani kwenye Ligi Kuu na itacheza na Timu iliyopanda Daraja Msimu huu Blackpool lakini kukosekana kwa Nasri ni pigo kwani kunaleta udhaifu kwenye Kiungo hasa kwa vile haijulikani kama Nahodha wao Cesc Fabregas ataweza kucheza mechi hiyo.
Anderson arudi mazoezini
Anderson ambae aliumia vibaya goti lake kwenye mechi na West Ham Mwezi Februari Mwaka huu yupo kwenye mazoezi makali na inategemewa ataonekana tena dimbani akiwa na Timu yake Manchester United Mwezi Septemba.
Maumivu hayo ya goti yalimfanya akose kuichezea Nchi yake Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Anderson, akiongea kwenye tovuti ya Man United, amesema: “Nina furaha kurudi baada ya Miezi 6 bila Soka. Najiskia vizuri na nipo kwenye mazoezi makali sasa. Sina tatizo tena na goti, nakimbia na kufanya mazoezi magumu sasa.”

No comments:

Powered By Blogger