CHEKI: www.sokainbongo.com
Wachezaji watano wa Ufaransa wako kiti moto!!!
Wachezaji watano waliokuwa Timu ya Ufaransa iliyocheza Kombe la Dunia huko Afrika Kusini leo watashuka mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FFF, Chama cha Soka France, kujibu shutuma za kuwa vinara wa mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini.
Wachezaji hao ni Nahodha Patrice Evra, Nicolas Anelka, Eric Abidal, Franck Ribery na Jeremy Toulalan.
France haikushinda hata mechi moja huko Afrika Kusini na ilimaliza Kundi lake ikiwa mkiani na Timu nzima iligoma kufanya mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa kufuatia kugombana na aliekuwa Kocha wao Raymond Domenech.
Wachezaji wote 23 walisimamishwa kucheza mechi ya kirafiki na Norway iliyochezwa Oslo Agosti 11 na France kufungwa na Norway 2-1 na hatua hiyo ilipendekewa na Kocha mpya Laurent Blanc.
Hata hivyo huenda Franck Ribery asiwepo kwenye kiti moto hicho baada ya Klabu yake Bayern Munich kukataa kumruhusu kwa vile wito huo uko nje ya Kalenda ya Kimataifa ya FIFA.
Ferguson ampa Tano Scholes!!!
Sir Alex Ferguson amemmiminia sifa Kiungo wake Veterani Paul Scholes baada ya kuwa ndio injini iliyoleta ushindi wa bao 3-0 hapo jana kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Newcastle Uwanjani Old Trafford.
Ferguson ametamka: “Ni mtoa pasi mzuri na ana akili ya mpira! Mtu yeyote anaecheza kiwango hicho kwa umri wake ni Mchezaji spesho!”
Scholes yupo Manchester United kwa Miaka 17 sasa na amechezea mechi 400 na kutwaa Ubingwa mara 9.
No comments:
Post a Comment