Saturday 21 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Wenger: ‘Scholes ni Mchezaji mzuri lakini Mcheza rafu!’
Bila shaka Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, huenda atamkera rafiki yake wa siku hizi Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, kwani alipohojiwa na Wanahabari Wenger alimsifia Veterani wa Man United Paul Scholes lakini pia akamponda kuwa ni Mchezaji anaecheza rafu nyingi.
Wenger, akihojiwa, alijibu: “Unaniuliza kama Scholes anacheza mchezo mzuri uwanjani, nitajibu hapana! Hucheza rafu sana!”
Mwaka jana, Wenger aliwahi kumsema Kiungo wa Man United, Darren Fletcher, kuwa katika mechi iliyochezwa Old Trafford na Man United kuichapa Arsenal alichezeshwa tu ili kucheza rafu tu na kuwasimamisha Arsenal.
Alipotajiwa kuwa Mchezaji wake wa zamani Patrick Viera alikuwa na rekodi mbovu ya kucheza rafu kupita Scholes, Wenger akang’ang’ania kuwa ingawa Scholes ni Mchezaji mzuri lakini ni mcheza rafu.
Mchina abwaga manyanga kuinunua Liverpool
Tajiri wa Hong Kong, Kenny Huang, amejitoa katika ununuzi wa Klabu ya Liverpool baada kuona ofa yake inazungushwa tu na kuwekewa mizengwe.
Mara baada ya Huang kutoa ofa ya kuinunua Liverpool kutoka kwa wenye mali Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gilleet, akaingia mnunuzi wa pili kutoka Syria Yahya Kirdi.
Liverpool ina madeni zaidi ya Pauni Milioni 350.
Wakati huo huo, Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, amesema huenda akamtoa kwa mkopo Alberto Aquilani ili arudi kwao Italia.
Aquilani alinunuliwa Mwaka jana kwa Pauni Milioni 20 ili kuchukua nafasi ya Xabi Alonso aliehama lakini ameshindwa kujizatiti Klabuni hapo na amekuwa akikumbwa na majeruhi mara kwa mara.

No comments:

Powered By Blogger