Wednesday 18 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

BEBE: ‘Toto la Mtaani’ lapanda chati hadi Old Trafford!!!!
Mwaka mmoja uliopita, Bebe, Miaka 20, jina kamili Tiago Manuel Dias Correja, alishiriki huko Bosnia Sherehe za Soka la Ulaya la Mtaani kwa Watu Wasio na Makazi akitokea kwenye Kituo cha Hifadhi ya Casa do Gaiato ambayo huwekwa Watu wasio na Makazi.
Mara baada ya kuwika huko Bosnia kwa kufunga mabao 40 katika Mechi 6 alizoichezea Timu ya Ureno ya Watu Wasio na Makazi, Bebe akachukuliwa na Timu ya Daraja la 3 Estrela Amadora na hapo akang’ara zaidi na kununuliwa na Vitoria Guimaraes, Timu ya Daraja la Juu.
Ndipo Sir Alex Ferguson akaletewa taarifa Bebe ni ‘lulu’ na Maskaunti wa Manchester United walio Ureno na taarifa hizo zilipigwa dole na aliekuwa Msaidizi wa Ferguson, Carlos Quieroz, ambae sasa ndie Kocha wa Ureno.
Baada ya Miezi mitatu tu kuwa na Vitoria Guimaraes, Bebe akatua Manchester United kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7.4.
Bebe ametamka: “Kutua Man United ni kutimia kwa ndoto! Kuwa na Wareno hapa ni motisha! Ronaldo aliwahi kucheza hapa. Nani na Anderson wapo hapa. Nataka kuwa kama wao!”
Anderson ni Mbrazil lakini wao huongea Kireno na pia amekulia Kisoka huko Ureno.
Nae Kocha wa Man United, Ferguson, ametamka: “Bebe ni kichocheo kwa Vijana wote ambao hawakujaliwa kuwa na mwanzo mzuri maishani. Ipo mifano mizuri ya Vijana wasiobarikiwa kuanza vizuri maisha yao na kisha wakafanikiwa. Wanachotakiwa ni kuwa na juhudi.”
Boateng anunuliwa na Genoa, aangukia AC Milan
Mchezaji wa Portsmouth, Kevin-Prince Boateng, ameuzwa kwa Klabu ya Italia Genoa wa ada ya Pauni Milioni 5 na mara tu baada ya kukamilika uhamisho huo akakopeshwa kwa AC Milan ambako atakaa kwa Msimu mmoja.
Boateng, miaka 23, aliiwezesha Ghana kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na alijiunga na Portsmouth Mwaka jana Mwezi Agosti akitokea Tottenham.

No comments:

Powered By Blogger