Monday 16 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Blatter ataka mabadiliko Kombe la Dunia
Sepp Blatter amesema FIFA inatafakari kuondoa matokeo ya sare kwenye Mechi za Makundi katika Fainali za Kombe la Dunia kwa Timu kupigiana penalti baada ya dakika 90 ikiwa ziko sare.
Rais huyo wa FIFA ametamka: “Penalti kwenye hatua za Makundi zitazimaliza Timu zinazocheza defensi tu. Pia tunafikiria kuondoa muda wa nyongeza wa Dakika 30 kwa Mechi za Raundi ya Pili na kuendelea kwa kurudisha lile goli la dhahabu. Hivyo Timu zikiwa sare Dakika 90 zitaongezwa muda na itayofunga bao ndio Mshindi na Mechi itasimama hapohapo!”
Sheria hiyo ya goli la dhahabu ilitumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Ufaransa Mwaka 1998 lakini Fainali iliyofuata ya Mwaka 2002 huko Japan na Korea Kusini ilifutwa.
Blatter anaamini mabadiliko hayo yataleta msisimko zaidi kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa kuziwekea ngumu Timu zinazotaka suluhu tu.
Fainali zinazofuata za Kombe la Dunia ni Mwaka 2014 huko Brazil.
Pia, Blatter alisistiza FIFA iko kwenye jitihadi ya kulipatia ufumbuzi suala la kutumia teknlojia ya kisasa ya kusaidia Marefa kutoa uamuzi sahihi na wa haraka juu ya mpira kuvuka mstari wa goli au la.
Blatter ametamka: “Pale tu tutakapopata mfumo salama, wa haraka na usio na utata, tutautumia!”
Suala hilo la kutumia teknolojia litajadiliwa Mwezi Oktoba kwenye Mkutano wa IFAB [International Football Association Board], chombo ambacho kinaijumuisha FIFA na Vyama vya Soka vya England, Wales, Scotland na Ireland ambavyo ndivyo vinachukuliwa kama Waanzilishi wa Soka na hivyo ndio wenye mamlaka ya kubadili Sheria za Soka Duniani.

No comments:

Powered By Blogger