Monday 16 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Gerrard amtetea Reina kwa kuipa zawadi Arsenal
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amemtetea Kipa wake Jose Reina kwa kosa lake kuipa Arsenal zawadi ya bao la kusawazisha dakika za mwisho za majeruhi hapo jana Uwanjani Anfield kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu kwa Timu hizo mbili.
Mechi hiyo ilikwisha kwa bao 1-1.
Gerrard ametamka: “Huyu ni Kipa mzuri na anatupa pointi nyingi. Ile ilikuwa bahati mbaya!”
Nahodha huyo wa Liverpool pia amedai Joe Cole alietolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Martin Atkinson kwa kumchezea rafu Beki wa Arsenal Laurent Koscielny, alikuwa na bahati mbaya kupewa Kadi hiyo na alidhani alistahili Njano badala yake.
Nae Beki wa Arsenal, Laurent Koscielny, alitolewa kwa Kadi Nyekundu mwishoni baada ya kupata Kadi za Njano mbili ndani ya dakika moja.
CAPELLO: Mwanzo wa mwisho umefika!
• FA yatangaza Meneja ataefuatia ni Mwingereza!
Mrithi wa Mtaliana Fabio Capello kama Kocha wa England atakuwa Mwingereza FA imetamka.
Mkataba wa Capello unamalizika 2012 ingawa kwa sasa yuko kwenye presha kubwa baada ya kutofanya vizuri kama wadau walivyotarajia huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
FA imesema wao wanategemea Capello atatumikia muda wake wote wa Mkataba na hivyo kuondoa dhana kuwa huenda akang’oka mapema.
England inategemewa kuanza kampeni za kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 Mwezi ujao watakapoanza mechi zao za Makundi.

No comments:

Powered By Blogger