Wednesday 18 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

FUNGUA PAZIA MSIMU MPYA 2010/11: NGAO YA HISANI
Yanga 3 Simba 1
Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Wapinzani wa Jadi, Yanga na Simba, walijimwaga dimbani katika pambano maalum la kufungua pazia ya Msimu mpya wa 2010/11 kugombea Ngao ya Hisani na Yanga walibuka kidedea kwa kuitwanga Simba kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya Timu hizo kwenda sare 0-0 hadi mwishoni mwa dakika 90.
Simba walikosa penalti 3 kati ya 4 zilizopigwa na kufunga moja tu.
Yanga walifunga penalti 3 na kukosa moja.
Fulham yamsaini Dembele
Fulham imekamilisha usajili wa Fowadi wa Kimataifa wa Ubelgiji Moussa Dembele ambae anachezea Klabu ya AZ Alkmaar kwa Mkataba wa Miaka mitatu.
Dembele, umri Miaka 23, amechukuliwa kwa ada ya Pauni Milioni 5 na amekuwa akiichezea Klabu ya Uholanzi AZ Alkmaar kwa Miaka mitatu.
Meneja wa Fulham, Mark Hughes, amefurahishwa kwa usajili huo kwani Birmingham pia ilikuwa ikimwania Mchezaji huyo.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Tottenham yachapwa 3-2
Klabu Ya Uswisi, Young Boys Berne, imewafunga Tottenham mabao 3-2 katika mechi ya kwanza ya Hatua ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI mjini Berne, Uswisi.
Timu hizo zitarudiana White Hart Lane, Jijini London, nyumbani kwa Tottenham, Jumatano ijayo.
Katika mechi nyingine za UEFA CHAMPIONS LIGI hapo jana, Zilina ya Slovakia ilifunga Slavia Prague 2-0, Ajax Amsterdam na Dynamo Kiev zilitoka sare 1-1 huko Kiev.
Rosenborg iliifunga FC Copenhagen 2-1 na Zenit St Petersburg iliishinda Auxerre 1-0.
Huko Uswisi, Young Boys walikuwa mbele kwa ba0 3-0 hadi dakika ya 28 kwa magoli kupitia Senad Lulic, Henri Bienvenu kutoka Cameroun na Xavier Hochstrasser.
Mabao ya Tottenham yalifungwa na Sebastien Bassong na Roman Pavlyuchenko.
Leo kutakuwa na mechi 5 za UEFA CHAMPIONS LIGI na marudio yake ni Jumanne ijayo.

No comments:

Powered By Blogger