Sunday 15 August 2010

Barca yatwangwa!!
Sevilla, ikiwa nyuma kwa bao 1-0 hapo jana, ilizinduka na kuibamiza FC Barcelona mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya Supercup, Kombe linaloshindaniwa na Bingwa wa La Liga na yule alienyakua Kombe la Mfalme huko Spain ikiwa Mechi za ufunguzi wa Msimu mpya.
Mechi ya marudiano itakuwa Nou Camp, Barcelona hapo Agosti 21.
Zlatan Ibrahimovic aliwapa Barca bao la kuongoza lakini Kipindi cha pili Sevilla walizinduka na Frederic Kanoute akapachika bao mbili na Luis Fabiano akafunga la tatu.
LIGI KUU: Leo ni Liverpool v Arsenal
Ni Bigi Mechi ambayo imeshangaza wengi kupangwa kuwa ndio Mechi ya kwanza kwa Msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa Timu za Liverpool na Arsenal zitakapokutana huko Anfield leo saa 12 jioni, bongo taimu.
Katika Mechi kama hii Msimu uliokwisha, Arsenal ilishinda bao 2-1.
Kwa jumla, Timu hizi zimeshacheza mara 173 na Liverpool wameshinda mara 68, Arsenal mara 60 na sare 44.
Lakini kwenye makutano yao kwenye historia ya Ligi Kuu, Liverpool wameshinda Mechi 3 kati ya 18 walizocheza.
Katika Mechi ya leo, Mastaa watakaokosekana ni Van Persie na Fabregas kwa Arsenal na Liverpool watamkosa Fernando Torres kwa vile wote bado sio fiti.
Refa katika Mechi ya leo atakuwa Martin Atkinson

No comments:

Powered By Blogger