CHEKI: www.sokainbongo.com
Vidic asaini Mkataba mpya Man United
Nemanja Vidic amesaini Mkataba mpya wa Miaka minne na Klabu yake Manchester United na hivyo kuondoa kabisa uvumi kuwa anahama.
Vidic alikuwa akiunganishwa na kuhamia AC Milan na Real Madrid.
Mara baada ya Vidic kusaini Mkataba huo huku mbele ya Mkurugenzi Mtendaji, David Gill, na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, Ferguson aliamka: “Hii inaua uvumi wote. Vidic ni sentahafi bora Ulaya na tumefurahi tutakuwa nae kwa Miaka mingi ijayo.”
Vidic alijiunga na Manchester United Januari 2006 kutoka Spartak Moscow na kuiwezesha Klabu yake, akiwa patna na Rio Ferdinand kwenye difensi, kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 3 pamoja na Ubingwa wa Ulaya Mwaka 2008.
Ireland aiponda Klabu yake ya zamani Man City!
Stephen Ireland ameishambulia vikali Manchester City, kuanzia Meneja wake Roberto Mancini na baadhi ya Wachezaji wa Timu hiyo ambao amesema wameheuka kwa fedha na hatua yake hiyo inafuatia kukasirishwa kwake kwa kulazimika kuhamia Aston Villa.
Ireland alilazimika kuondoka Man City kwenda Aston Villa ikiwa ni makubaliano ya Klabu hizo mbili ili kukamilisha uhamisho wa James Milner kutoka Aston Villa kwenda Man City.
Miongoni mwa maneno ya Ireland, Miaka 24, ambae alianzia Soka lake hapo Man City tangu akiwa na Miaka 15, ni pamoja na kudai:
• James Milner atapata mstuko akitua Man City kwani huko si kuzuri kama anavyotarajia.
• Amedai Meneja Mancini hana uhusiano mzuri na Wachezaji wake.
• Ireland amejigamba yeye ni sawa au mzuri zaidi ya Wachezaji wapya waliosainiwa na Man City Msimu huu.
• Wachezaji wapya wa Man City wanaheuka kwa fedha na kuvaa Saa za mkononi za bei mbaya za zaidi ya Pauni 10,000.
• Wachezaji wa Man City hawatambui tena uaminifu na utiifu kwa Klabu hiyo.
• Alimponda Mancini kwa kumbeza na kwamba amesahau yeye siku zote alikuwa Mchezaji bora mazoezini.
Ireland pia alisema: “Nimefika Villa na nimeshangazwa. Ni Klabu ya kifamilia, kila Mtu ni mstaarabu. Ni tofauti na Man City.”
No comments:
Post a Comment