CHEKI: www.sokainbongo.com
LIGI KUU BARCLAYS: Man United 3 Newcastle 0
Manchester United, wakiwa nyumbani Old Trafford, wameanza kampeni yao ya kurudisha taji, kwa kuichapa ‘Timu mpya’ Newcastle mabao 3-0.
Katika Msimu wao wa mwisho Ligi Kuu Mwaka 2008/9 kabla kushushwa Daraja, Newcastle waliweza kutoka sare 1-1 na Man United hapo Old Trafford lakini leo Jumatatu usiku Agosti 16, katika mechi yao ya kwanza tangu wapande Daraja, walikuta habari mpya.
Wakicheza huku wakiwa na Mtu 9 nyuma na kumwacha Straika wao Carroll ahahe peke yake mbele, Newcastle walidumu hadi dakika ya 33 na ndipo Dimitar Berbatov alipowatoboa kwa bao la kwanza.
Bao la pili la Man United lilifungwa na Darren Fletcher baada ya ujanja wa Rooney.
Wakongwe Scholes na Giggs walishirikiana vyema na kusababisha bao la tatu kupitia Giggs dakika ya 85.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumapili ijayo ugenini dhidi ya Fulham.
Vikosi vilivyoanza:
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Fletcher, Scholes, Nani, Berbatov, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Rafael Da Silva, Smalling, Carrick, Giggs, Macheda, Hernandez.
Newcastle: Harper, Perch, Coloccini, Williamson, Jose Enrique, Routledge, Smith, Nolan, Barton, Gutierrez, Carroll.
Akiba: Krul, Ryan Taylor, Xisco, Ameobi, Vuckic, Ranger, Tavernier.
Refa: Chris Foy
Almunia kuondoka Ze Gunners!!
Manuel Almunia amekiri kuwa itamlazimu aondoke Arsenal ikiwa Klabu hiyo itamleta Kipa mwingine.
Kumekuwa na taarifa kuwa Arsenal iko mbioni kumchota Kipa wa Fulham Mark Shwarzer au Shay Given toka Manchester City kwa vile Makipa wa Arsenal Almunia na mwenzake Fabianski hawaaminiki.
Almunia ndie aliecheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya sare 1-1 na Liverpool hapo Jumapili na Wadau kumlaumu kwa bao la Liverpool.
Almunia ameungama kuwa ni ngumu kwake kuwa makini huku kuna taarifa kila kona kuwa Kipa mpya atatua Emirates.
No comments:
Post a Comment