Friday 20 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kocha Ureno, Queiroz afungiwa Siku 30
Kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Carlos Queiroz, amefungiwa Siku 30 na Chama cha Soka cha Ureno kwa kuwatukana Wakaguzi wa Madawa yaliyopigwa marufuku kwa Wachezaji ambao walikwenda Kambini Nchini Ureno kuwakagua Wachezaji wa Ureno wakati wakijitayarisha kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Queiroz atakosa kuisimamia Timu yake kwa mechi za Makundi kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 ambazo Ureno watacheza na Cyprus Septemba 3 na Norway siku nne baadae.
Pia, Kocha huyo amepigwa Faini ya Dola 1280.
Kamati ya Nidhamu ya Chama cha Soka cha Ureno, FPF, ilimwona ana hatia ya kutoa matusi lakini haikumkuta na hatia na kosa la kutaka kuwazuia Wakaguzi hao kufanya kazi yao ambalo ni kosa kubwa zaidi na, pengine, lingemfanya amwage unga.
Katika utetezi wake, Queiroz aliita Mashahidi kadhaa, akiwemo Sir Alex Ferguson, alieruka hadi Lisbon, Ureno kutetea tabia njema ya Msaidizi wake wa zamani wa huko Old Trafford.

No comments:

Powered By Blogger