Thursday 19 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Ulaya kuwaka moto leo!
• Rapid Vienna v Aston Villa
• FC Timisoara v Man City
• Liverpool v Trabzonspor
Timu 3 za Ligi Kuu England, Aston Villa, Liverpool na Man City, leo ni miongoni mwa lundo la Timu za Ulaya zitakazocheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ili kuwania kuingia Hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI.
Marudio ya mechi za leo ni Wiki ijayo Alhamisi, Agosti 26.
Liverpool wataanza mechi ya leo wakiwa nyumbani Anfield dhidi ya Trabonspor ya Uturuki lakini watacheza bila ya Javier Mascherano ambae aliumia siku ya Jumapili walipotoka sare na Arsenal ya 1-1 kwenye Ligi Kuu.
Lakini, pengine, sababu kubwa ya kutomchezesha Mascherano ni kumlinda thamani yake isipungue kwani inajulikana Mascherano anataka kuhama Liverpool na akicheza leo, Klabu yake mpya haItaruhusiwa kuMchezesha Mashindano ya Ulaya.
Aston Villa na Manchester City zitakuwa ugenini huku Villa wakiwa Austria Uwanja wa Gerhard Happi dhidi ya Rapid Vienna na watacheza bila ya Richard Dunne, aliefungiwa, John Carew, Gabriel Agbonlahor, Carlos Cuellar na James Collins ambao ni majeruhi.
Man City wao wapo Uwanja wa Dan Paltisanu huko Romania kucheza na FC Timisoara na Mchezaji mpya, Supa Mario, Mario Balotelli, huenda akacheza mechi yake ya kwanza.
Ze Gunners mbioni kumnasa Beki Squillaci
Klabu ya Sevilla ya Spain imethibitisha Arsenal na wao wapo mazungumzoni ili Senta hafu wao kutoka Ufaransa, Sebastien Squillaci, ahamie Emirates.
Squillaci aliachwa na Sevilla kwenye Kikosi chao kilichocheza na Braga kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ili kumfanya asizuiwe kuichezea Arsenal akihamia huko.
Arsenal wapo sokoni kutafuta Beki ili kuziba mapengo yaliyoachwa na William Gallas, Sol Campbell, Mikel Silvestre na Philippe Senderos ambao wote walimaliza Mikataba yao.
Tayari Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameshanunua Senta Hafu mmoja kutoka Ufaransa ambae ni Laurent Koscielny aliecheza mechi ya Ligi Kuu Jumapili na Liverpool na kutwangwa Kadi Nyekundu.
Squillaci alihamia Sevilla Mwaka 2008 akitokea Lyon.
Liverpool wadai Mascherano atang’oka kwa dau nono!
Kocha wa Liverpool, Roy Hodgson, amesisitiza Kiungo wao kutoka Argentina ataruhusiwa kuondoka Liverpool ikiwa Timu inayomtaka itatoa dau zuri na linalostahili kwa thamani yake.
Mascherano, Miaka 26, ambae ndie Nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina, bado amebakiza Miaka miwili kwenye Mkataba wake na Liverpool lakini mwenyewe amekuwa akitaka kwenda Inter Milan kuungana tena na aliekuwa Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, ambae yuko huko.
Mascherano ameichezea Liverpool mara 138 tangu ahamie hapo kutoka West Ham Mwaka 2007.

No comments:

Powered By Blogger