Friday 20 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Mechi za Wikiendi hii
[Saa za Bongo]
Jumamosi, 21 Agosti 2010
[Saa 11 jioni]
Arsenal v Blackpool
Birmingham v Blackburn
Everton v Wolverhampton
Stoke v Tottenham
West Brom v Sunderland
West Ham v Bolton
[Saa 1 na robo usiku]
Wigan v Chelsea
Jumapili, 22 Agosti 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Newcastle v Aston Villa
[Saa 12 jioni]
Fulham v Man Utd
Jumatatu, 23 Agosti 2010
[Saa 4 usiku]
Manchester City v Liverpool
TATHMINI:
Timu iliyopanda Daraja, Blackpool, itatua Uwanja wa Emirates wakitafuta ushindi wao wa pili katika mechi mbili za Ligi Kuu baada ya kuichapa Wigan 4-0 lakini kazi hiyo itakuwa ngumu kwa vile Wenyeji wao ni Arsenal ambao wanatafuta ushindi wao wa kwanza baada ya kwenda sare 1-1 na Liverpool katika mechi ya kwanza.
Katika mechi hii, huenda Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, akaonekana Uwanjani baada ya kuwa majeruhi.
Baada ya kipigo cha 3-2 ugenini kwenye mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI walichokipata huko Uswisi toka kwa Young Boys siku ya Jumanne, Tottenham wataingia tena ugenini kucheza na Stoke City waliofungwa na Wolves kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu.
Kwenye mechi ya kwanza ya Ligi, Wigan walinyukwa 4-0 na Blackpool na kesho wapo nyumbani Uwanja wa DW kucheza na Mabingwa wa Ligi Kuu Chelsea ambao waliwatandika West Bromwich Albion mabao 6-0.
Msimu uliokwisha, kwenye mechi kama hii, Wigan waliifunga Chelsea.
West Bromwich Albion, baada ya kipigo cha 6-0 huko Stamford Bridge, watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sunderland ambao katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Birmingham waliongoza 2-0 lakini wakawaruhusu Birmingham kusawazisha na mechi kwisha 2-2.
West Ham watakuwa kwao Upton Park kucheza na Bolton Wanderers na safari hii wataombea ushindi baada ya kufungwa 3-0 na Aston Villa kwenye mechi ya kwanza.
Bolton walitoka sare 0-0 na Fulham kwenye mechi ya ufunguzi.
Baada ya kuchapwa 1-0 na Blackburn huko Ewood Park, Everton watakuwa nyumbani Goodison Park kucheza na Wolves ambao walishinda mechi ya kwanza 2-1 dhidi ya Stoke City.
Katika Uwanja wa Mtakatifu Andrew, Birmingham watawakaribisha Blackburn Rovers na pambano hili litakuwa gumu hasa kwa vile Birmingham wana rekodi nzuri Uwanjani kwao ya kutofungwa katika mechi zao 15 za mwisho za Ligi Kuu.
Mechi ya kwanza ya Jumapili ni kati ya Newcastle United v Aston Villa Uwanjani St James.
Hii ni mechi ya kwanza ya Uwanja wa nyumbani kwa Newcastle tangu wapande Daraja kurudi tena Ligi Kuu na ni muhimu hasa baada ya kupigwa 3-0 na Manchester United wiki iliyokwisha.
Aston Villa wanaingia kwenye mechi hii wakitoka kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham.
Mechi ya pili ya Jumapili ni huko Craven Cottage ambako Fulham watacheza na Manchester United ambao katika Misimu miwili iliyopita wamekuwa wakifungwa kila wanapotua Craven Cottage.
Jumatatu usiku, Uwanjani City of Manchester, Timu Tajiri iliyonunua Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu huu kwa jumla ya Pauni Milioni 126, Manchester City wataivaa Liverpol kwenye mechi inayongojewa kwa hamu na Wadau wengi.

No comments:

Powered By Blogger