BLACKBURN 1 v HULL CITY 1
LIVERPOOL 2 v MIDDLESBROUGH 1
NEWCASTLE 1 v BOLTON 0
STOKE CITY 3 v ASTON VILLA 2
TOTTENHAM 1 v SUNDERLAND 2
WEST BROM 1 v EVERTON 2
RIPOTI ZA MECHI KWA UFUPI:
West Brom 1-2 Everton
Magoli ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Leon Osman na Ayegbeni Yakubu yaliwapa ushindi Everton waliocheza ugenini dhidi ya West Brom.
Bao la West Brom lilifungwa dakika ya 89 na Bednar kwa njia ya penalti.
Blackburn 1-1 Hull
Timu iliyopanda daraja msimu huu Hull City wamezidi kugangamara na kutoka suluhu ugenini ya bao 1-1 na Blackburn.
Jason Roberts wa Blackburn aliua mtego wa kuotea na kufunga bao dakika ya 39 lakini Hull City wakasawazisha muda mfupi baadae kupitia Richard Garcia aliefunga kwa kichwa.
Katika mechi yao ya kwanza LIGI KUU Hull City waliwafunga Fulham 2-1.
Liverpool 2-1 Middlesbrough
Steven Gerrard alipiga mkwaju mkali katika dakika za majeruhi na kufunga bao la ushindi kwa Liverpool ambao wengi walitegemea wamekufa nyumbani kwao baada ya Mido kuwapa bao la kuongoza Middlesbrough katika dakika ya 70 lililodumu hadi dakika ya 86 wakati shuti la Jamie Carragher lilipombabatiza Nahodha wa Boro Emmanuel Pogatetz na kuwasawazishia Liverpool.
Huu ni ushindi wa pili kwa Liverpool kwani wiki iliyopita walishinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Sunderland.
Newcastle 1-0 Bolton
Michael Owen alitokea benchi la akiba na kuingizwa uwanjani kwenye dakika ya 53 alifunga bao la ushindi dakika ya 71 na kufanya mechi Newcastle 1 Bolton 0.
Katika mechi yao ya kwanza ya LIGI KUU Newcastle walilazimisha sare ya 1-1 na Man U walipocheza Old Trafford nyumbani kwa Mabingwa hao wa LIGI KUU.
Stoke City 3-2 Aston Villa
Mamady Sidibe aliwapatia Stoke City bao la tatu na la ushindi katika dakika za majeruhi kwenye vuta nikuvute walipocheza na Aston Villa.
MAGOLI YA STOKE CITY: Lawrence dakika ya 30 kwa penalti, Fuller 80, Sidibe 90.
MAGOLI YA ASTON VILLAs: Carew 63, Laursen 84.
No comments:
Post a Comment