Tuesday 19 August 2008

ARGENTINA NAO WAJIKITA FAINALI YA SOKA OLIMPIKI!
Argentina 3 Brazil 0 !!!!!
Ni mechi ambayo wapenzi wengi wa Brazil wanaamini Refa kutoka Uruguay hawakuwatendea haki pale aliporuhusu bao la kwanza lililofungwa kwa mkono, la pili la kuotea na la tatu la penalti tata na vilevile kuwanyima bao lao safi!!
Lakini juu ya yote ni pale Refa huyo wa Uruguay kuwapa wachezaji wawili wa Brazil kadi nyekundu huku watani wa jadi Argentina wakicheza rafu ambazo Refa alizipeta tu!
Hii ina maana Nigeria watakutana na Argentina kugombea Medali ya Dhahabu kwenye Fainali na atakaefungwa mechi hii atapata Medali ya Fedha.
Brazil watamenyana na Belgium kwenye patashika ya Medali ya Shaba.

No comments:

Powered By Blogger