Thursday 21 August 2008

Man City wamchukua Kompany
Manchester City wameafikiana na Klabu ya Hamburg ya Ujerumani kumnunua Mlinzi wa Kibelgiji Vincent Kompany [22] ambae ameshaichezea Timu ya Taifa ya Ubelgiji mara 23.
Mpaka sasa Meneja wa Man City Mark Hughes ameshawasaini Mbrazil Jo kutoka CSKA Moscow na Tal Ben Haim kutoka Chelsea.
SUNDERLAND WAPATA WA PILI SIKU MOJA!!!
Sunderland wamemnunua David Healy kutoka Fulham kwa mkataba wa miaka mitatu na anakua Mchezaji wa pili kuchukuliwa na Klabu hiyo kwa leo baada ya Djibril Cisse kusaini leo kwa mkopo.
Meneja wa Sunderland amesema anamfahamu David Healy tangu alipoanza kucheza Man U na anaamini atasaidia sana Sunderland.

No comments:

Powered By Blogger