Sunday 17 August 2008

MAN U 1 NEWCASTLE 1
Mabingwa wa LIGI KUU UINGEREZA Manchester United wameanza kampeni ya kutetea ubingwa wao kwa suluhu ya 1-1 na timu ya Newcastle kwenye uwanja wao wa Old Trafford.
Ingawa Man U walitawala dakika 20 za mwanzo na kukosa mabao kadhaa ya wazi Newcastle ndio waliopata bao kwanza wakati Mnigeria Obafemi Martins alipofunga kwa kichwa kufuatia mpira wa kona.
Bao hili lilidumu dakika moja tu na Darren Flrtcher akarudisha baada ya muvu nzuri ya Mabingwa hao.
Baada ya hapo Man U walipata pigo pale kiungo Michael Carrick alipoumia na kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na John O’Shea.
Kipindi cha pili Man U iliwaingiza chipukizi wawili kutoka Brazil ambao ni Rodrigo Possebon na Rafael Da Silva. Vijana hao. Mbali ya Man U kutoshinda, walionyesha ni wachezaji wenye vipaji.
Mchezaji tegemeo Carlos Tevez hakuwepo kwenye timu kwa sababu amerudi kwao Argentina baada ya kupata msiba kwenye familia.
Man Utd: Van der Sar, Brown, Vidic, Ferdinand, Evra, Fletcher, Carrick, Scholes, Giggs, Campbell, Rooney. AKIBA: Kuszczak, Neville, Rafael Da Silva, O'Shea, Evans, Gibson, Possebon.

Newcastle: Given, Beye, Taylor, Coloccini, N'Zogbia, Milner, Butt, Guthrie, Gutierrez, Duff, Martins. AKIBA: Harper, Jose Enrique, Bassong, Smith, Geremi, Edgar, Donaldson.

No comments:

Powered By Blogger