Sunday 17 August 2008

ARSENAL WAUZA MWINGINE!
Beki wa Arsenal Justin Hoyte ameuzwa kwa klabu ya Middlebrough kwa Pauni milioni 3.
Beki huyu Mwingereza mwenye umri wa miaka 23 alianza kuchezea Arsenal tangu timu ya watoto na amecheza jumla ya mechi 68 kwenye kikosi cha kwanza tangu msimu wa 2002/3 ingawa hakuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi hicho.
Wachezaji wengine waliouzwa msimu huu na klabu walizoenda pamoja na dau lao kwenye mabano ni Gilberto Silva (Panathinaikos, £1m), Alexander Hleb (Barcelona, £11.8m), Jens Lehmann (Stuttgart, bure-mkataba uliiisha) na Mathieu Flamini (AC Milan, bure-mkataba uliisha)

No comments:

Powered By Blogger