Monday, 18 August 2008

Carrick nje ya uwanja wiki 3
Kiungo wa Manchester United Michael Carrick atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia enka kwenye mechi ya jana dhidi ya Newcastle ambayo iliisha kwa bao 1-1.
Carrick alitoka nje ya kiwanja kwenye dakika ya 25 ya mechi.
Hii ina maana mchezaji huyu atazikosa mechi za Man U mbili ya kwanza ni ya LIGI KUU tarehe 25 Agosti dhidi ya Portsmouth.

Ya pili ni ya tarehe 29 Agosti 2008 itakayochezwa huko Monaco kugombea European Super Cup dhidi ya Klabu ya Kirusi Zenit St Petersburg ambao ni Mabingwa wa Kombe la UEFA. Super hushindaniwa kati ya Bingwa wa LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA na Bingwa wa Kombe la UEFA.
Carrick sasa anajumuika kwenye listi ndefu ya Wachezaji wa Man U ambao hawataonekana uwanjani kwa muda kutokana na sababu mbalimbali.

Kwenye mechi hiyo hiyo ya jana Ryan Giggs na chipukizi Frazier Campbell waliumia na ilibidi watolewe.
Wengine ambao hawakuwepo na hawatakuwepo ni Cristiano Ronaldo, Louis Saha, Park Ji-Sung and Owen Hargreaves ambao wote ni majeruhi, Nani amefungiwa mechi mbili, Anderson yuko na Timu ya Brazil kwenye michuano ya Olympic na Carlos Tevez yuko Argentina kwenye msiba wa familia.

No comments:

Powered By Blogger