Mshambuliaji wa Klabu ya Ufaransa Marseille Djibril Cisse leo anapimwa afya ili aweze kuhamia Klabu ya Sunderland kwa mkopo. Marseille imetangaza jana kuwa wamefikia makubaliano na Sunderland.
Cisse alichezea timu ya Liverpool iliyochukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2006 na ashawahi kuvunjika miguu yote miwili alipokuwa na Liverpool na hivyo kukosa kuichezea Ufaransa kwenye Kombe la Dunia mwaka 2006.
Sunderland inayoongozwa na Meneja Roy Keane, Nahodha wa zamani wa Man U, ishawasajili msimu huu Wachezaji wapya watatu kutoka Tottenham yaani Teemu Tainio, Steed Malbranque na Pascal Chimbonda na vilevile El Hadji Diouf kutoka Bolton.

No comments:
Post a Comment