Thursday 21 August 2008

MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA: UINGEREZA 2 CZECH 2 Katika dakika za majeruhi Joe Cole alifunga goli na kuwaokoa Uingereza kutoka kwenye kipigo na kufanya mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Wembley, London hapo jana iishe 2-2.
Goli la kwanza lilifungwa na Milan Baros wa Czech dakika ya 22 na Wes Brown akasawazisha dakika ya 45. Dakika ya 48 Czech wakapata bao la pili lililodumu hadi dakika ya 90 Joe Cole aliposawazisha.
Uingereza ambayo iliwakatisha Washabiki wake hiyo jana kwa mchezo mbovu itaanza kampeni yake ya kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi ujao kwa mechi dhidi ya Andorra tarehe 6 Septemba na tarehe 10 Septemba wanacheza na Croatia.
UINGEREZA: James, Brown, Ferdinand (Woodgate 57), Terry, Ashley Cole, Beckham (Jenas 79), Barry, Lampard (Bentley 79), Gerrard (Joe Cole 57), Defoe (Heskey 46), Rooney (Downing 69).AKIBA: Robinson, Hart, Johnson, Bridge, Upson, Walcott.
MAGOLI: Brown 45, Joe Cole 90.
Czech Republic: Cech, Grygera (Pospech 46), Ujfalusi, Rozehnal, Jankulovski, Vlcek (Jarolim 46), Kovac (Rajnoch 75), Polak, Plasil (Papadopulos 90), Sirl (Kadlec 75), Baros (Sverkos 46).AKIBA: Zitka.
MAGOLI: Baros 22, Jankulovski 48.
WATAZAMAJI: 69,738
REFA: Terje Hauge (Norway).


Mikael Silvestre wa MAN U anunuliwa ARSENAL

Mlinzi wa siku nyingi wa Manchester United jana amenunuliwa na Arsenal kwa kitita kisichojulikana.
Silvestre [31] alijiunga na Man U Septemba 1999 na alikuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Man U ingawa ilikuwa dhahiri asingeongezewa muda na klabu hiyo.
Tangu Patrice Evra ajiunge Man U kutoka Monaco mwaka 2006 Silvestre amekuwa akikosa namba timu hiyo.
Silvestre amechezea mechi 249 za LIGI KUU kwa timu ya Man U na ni mchezaji wa kwanza kuuzwa kwa Arsenal tangu alipouzwa Brian Kid mwaka 1974.


No comments:

Powered By Blogger