Saturday 23 August 2008

ARGENTINA DHAHABU OLIMPIKI!!!!!!
Timu ya soka ya Argentina leo imechukua Medali ya Dhahabu kwenye soka ya Wanaume baada ya kuwafunga Nigeria bao 1-0 katika mechi iliyoanza saa moja asubuhi saa za bongo na kuchezwa kwenye joto kali kiasi cha kufanya Refa aisimamishe rasmi mara mbili ili wachezaji wanywe maji.
Goli la ushindi la Argentina lilifungwa na Mshambuliaji wa Benfica Angel de Maria [pichani] katika dakika ya 58.
Hivyo Nigeria wameambulia Medali ya Fedha na Brazil jana walipata Medali ya Shaba baada ya kuwafunga Belgium 3-0.
Kwa upande wa Wanawake, USA wameshinda Medali ya Dhabu, Brazil Fedha na Ujerumani Shaba.

No comments:

Powered By Blogger