Monday 18 August 2008

SOKA OLYMPIC BEIJING 2008
Wakati kesho ni mechi za Nusu Fainali za Soka upande wa Wanaume leo timu za Soka za Wanawake za Brazil na USA zimetinga Fainali.
Timu ya Wanawake ya Brazil ikiongozwa na Mchezaji Bora wa Dunia kwa Wanawake Marta [pichani] leo iliwabamiza Mabingwa wa Dunia wa Wanawake Ujerumani kwa mabao 4-1. Nao Mabingwa watetetezi wa Olympic upande wa Wanawake USA waliwafunga Japan 4-2 katika Nusu Fainali nyingine.
Kesho saa 7 mchana saa za bongo Nusu Fainali ya kwanza upande wa Wanaume itachezwa kati ya Nigeria na Belgium.
Saa 10 jioni watani wa jadi Brazil na Argentina watashuka dimbani.
Fainali ni tarehe 23 Agosti 2008.

No comments:

Powered By Blogger