KWA HABARI MOTOMOTOZ, TAMU NA ZENYE UTAFITI WA KINA, TEMBELEA:
www.sokainbongo.com
Liverpool yapata Mnunuzi lakini……………………..
Klabu ya Liverpool iko mbioni kuuzwa kwa Wamiliki wa Timu maarufu ya mchezo wa Beziboli huko Marekani iitwayo Boston Red Sox lakini huenda hatua hii ikakwama kufuatia kufukuta kwa mgogoro ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Liverpool ambapo Wamiliki wa Liverpool, Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillett, wanataka kuwatimua Mkurugenzi Mtendaji, Christian Purslow na Mkurugenzi wa Masoko, Ian Ayre, ambao Wamiliki hao wanawaona kama kikwazo kwa Klabu hiyo kupata Mnunuzi.
Wakurugenzi hao wawili tayari wameshatafuta hifadhi ya Kisheria ili wasitimuliwe Liverpool na hatua hii huenda ikachelewesha uuzwaji wake.
Inasemekana Wamiliki hao wa Boston Red Sox wametoa ofa ya Pauni Milioni 300 ambayo inatosha kulipia deni la Pauni Milioni 240 la Liverpool pamoja na ada za benki ya Royal Bank of Scotland waliodhamini mkopo huo na ada hiyo ni Pauni Milioni 40.
Deni hilo pamoja na ada ya Benki ni lazima zilipwe kabla ya Oktoba 15 la sivyo Klabu hiyo itatozwa faini ya Pauni Milioni 60.
Ni muda mrefu sasa Liverpool imekuwa sokoni kutafuta mnunuzi lakini Watu wamekuwa wakikwepa kuinunua na wenye mali, Hicks na Gillett, wanahisi kikwazo ni hao Wakurugenzi wawili ambao sasa wanataka kuwatimua.
Hicks na Gillett waliinunua Liverpool Mwaka 2007 kwa Pauni Milioni 174.1 na kurithi deni la Pauni Milioni 44.8 tu.
Mimiliki Mkuu wa Boston Red Sox ni John W. Henry ambae pia anamiliki Kampuni nyingine kadhaa za michezo huko Marekani.
Huddlestone apona rungu la UEFA
Kiungo wa Klabu ya Tottenham HotspurTom Huddlestone amenusurika kuadhibiwa na UEFA baada ya kudaiwa kumpiga kiwiko Mchezaji wa FC Twente Marc Janko kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumatano iliyopita huko White Hart Lane ambayo Spurs walishinda bao 4-1.
Janko alidai Huddlestone alikusudia kumpiga kipepsi wakati Wachezaji hao walipovaana katika tukio ambalo Refa alipiga filimbi kuashiria ni Janko ndie aliecheza faulo.
UEFA ilithibitisha kutaka kuchunguza mikanda ya tukio hilo na sasa imetamka baada ya kufanya hivyo Idara yao ya Nidhamu imeamua Huddlestone hakuwa na kesi ya kujibu na hivyo kupona kuadhibiwa.
No comments:
Post a Comment