Sunday, 3 October 2010

Chelsea wajikita kileleni!
• Chelsea 2 Ze Gunners 0
Bao moja kila kipindi yamewapa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Chelsea ushindi wa mabao 2-0 juu ya Arsenal Uwanjani Stamford Bridge katika mechi ya tatu ya leo ya Ligi na kuwafanya wajikite uongozini kwa pointi 4 mbele ya Manchester City walio nafasi ya pili, pointi 5 mbele ya Man United na pointi 7 mbele ya Arsenal huku Timu zote zikiwa zimecheza mechi 7.
Kama kawaida yao, Arsenal ndio walikuwa na umiliki bora wa mpira lakini ni Chelsea ndio walioleta mpasuko kwenye ngome ya Arsenal.
Alikuwa Didier Drogba aliefunga bao la kwanza dakika ya 39 alipoiwahi krosi ya Ashley Cole na kumhadaa Kipa Lukasz Fabianski.
Na bunduki kali ya Alex kutoka friki ya mita kama 30 hivi kwenye dakika ya 85 ilizaa bao la pili na kuifanya Stamford Bridge yote indirime kwa furaha.
Vikosi vilivyoanza:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Alex, Terry, Cole, Mikel, Essien, Ramires, Malouda, Anelka, Drogba.
Akiba: Turnbull, Zhirkov, Ferreira, Sturridge, Van Aanholt, Kakuta, McEachran.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Koscielny, Squillaci, Clichy, Diaby, Nasri, Wilshere, Song, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Szczesny, Rosicky, Vela, Denilson, Djourou, Eboue, Emmanuel-Thomas.
Refa: Mike Dean
MATOKEO MECHI ZA LEO:
Manchester City 2 Newcastle 1
Liverpool 1 Blackpool 2
Chelsea 2 Arsenal 0
Baada ya matokeo ya leo, Msimamo kwa Timu za juu ni:
1 Chelsea pointi 18
2 Man City pointi 14
3 Man United pointi 13
4 Arsenal pointi 11
5 Tottenham pointi 11
6 West Brom pointi 10
7 Stoke pointi 10
8 Villa pointi 10
9 Blackpool pointi 10
10 Fulham pointi 9

No comments:

Powered By Blogger