Tuesday 5 October 2010

PITIA TOVUTI BOMBA: www.sokainbongo.com

Newcastle yageuka mbogo, yataka De Jong aadhibiwe!
Newcastle imewaandikia FA kuwataka wamchukulie hatua Mchezaji wa Manchester City Nigel de Jong kwa kumvunja mguu Hatem Ben Arfa wa Newcastle katika mechi ya Ligi Kuu ambayo Man City walishinda 2-1 siku ya Jumapili.
Vilevile, Klabu hiyo imeitaka FA kuangalia uchezeshaji wa Refa Martin Atkinson ambae hakupiga filimbi ya faulo wakati Ben Arfa anavunjwa mifupa yote miwili ya mguuni na hivyo kutomwadhibu Mholanzi huyo.
Pia Newcastle wamedai Refa Atkinson aliwapa Man City penati ya utata ambayo Carlos Tevez aliwafungia bao la kwanza na wao kunyimwa penati ya wazi.
Kitendo cha de Jong kumvunja Ben Arfa kilimfanya Kocha wa Uholanzi, Bert van Marwijk, kutomwita Mchezaji huyo kwenye Timu yake itakayocheza mechi za EURO 2012 dhidi ya Moldova na Sweden wiki hii na ijayo.
Marwijk ameelezea tukio hilo kama ni baya na halistahili.
Romario atinga siasani, sasa ni Seneta!
Gwiji la Soka la zamani la Brazil, Romario, ameshinda uchaguzi huko Brazil kwa kupata kura zaidi ya Laki 150 na hivyo kuchaguliwa kuwa Seneta wa Bunge dogo la Shirikisho la Brazil kupitia Chama cha Kisoshalisti cha Brazil.
Romario, akigombea huku akinadi ilani yake ya kuendeleza miradi ya michezo kwa jamii masikini, alisheherekea ushindi huo kwa bonge la pati ya usiku kucha.
Romario aliwahi kuwa Mchezaji Bora wa Dunia Mwaka 1994 na ameshazichezea Klabu za Barcelona, Valencia, Flamengo na Vasco da Gama.
Mshauri wa Romario kwenye siasa, Marcio Saraiva, ametamka hapo baadae wanaweza kugombea Uraisi wa Brazil kwani hamna sababu ya kutofanya hivyo ikiwa Rais wa sasa wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, alianza kama mfua vyuma.

No comments:

Powered By Blogger