Ureno, Spain, Germany zapeta EURO 2012
Katika mechi za Makundi za EURO 2012, Germany ilipata ushindi mzuri wa 3-0 dhidi ya Uturuki huko Berlin na Urusi ilipata mshimshike huko Dublin, Republic of Ireland na hatimaye kushinda 3-2.
Ureno, iliyokuwa ikisuasua, ilizinduka na kuichapa Timu ngumu Denmark mabao 3-1 na Spain iliichapa Lithuania 3-1 ugenini.
Katika mechi ya Germany, Miroslav Klose aliifungia Germany mabao mawili na Mesut Oezil alifunga bao moja lakini hakushangilia bao hilo hata chembe kwani Uturuki ndiko wanakotoka Wazazi wake.
Belgium iliishinda Kazakhstan mabao mawili ugenini na bao zote zilipachikwa na Ogunjimi ambae awali aliamua kuichezea Nigeria anakotoka Baba yake lakini baadae akageuza mawazo na kuichezea Belgium alikozaliwa.
Katika mechi ya Ureno na Denmark, Nani wa Manchester United alifunga bao mbili ndani ya dakika mbili kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili Beki wa Ureno, Ricardo Carvalho, alijifunga mwenyewe na kuifanya mechi iwe 2-1.
Ronaldo aliwakikishia Ureno ushindi alipofunga bao la 3 dakika ya 85 na kuifanya Denmark ilale 3-1.
Katika Kundi C, Ireland ya Kaskazini ikicheza nyumbani Mjini Belfast iliibana mbavu Italy na kwenda nao sare 0-0.
Mabingwa wa Dunia, Spain, wakiwa ugenini, waliichapa Lithuania 3-1 kwa mabao mawili ya Fernando Llorente na David Silva.
Boa la Lithuania lilifungwa na Davydas Sernas.
Leo, kutakuwa na mechi mbili, France v Romania na Israel v Croatia.
Jumanne kutakuwa na lundo la mechi za Euro 2012 ikiwemo ile ya England v Montenegro.
EURO 2012:
Ratiba
Jumamosi, 9 Oktoba 2010
France v Romania
Israel v Croatia
Matokeo
Ijumaa, 8 Octoba 2010
Armenia 3 Slovakia 1
Kazakhstan 0 Belgium 2
Andorra 0 FYR Macedonia 2
Georgia 1 Malta 0
Hungary 8 San Marino 0
Cyprus 1 Norway 2
Czech Republic 1 Scotland 0
Luxembourg 0 Belarus 0
Albania 1 Bosnia-Hercegovina 1
Austria 3 Azerbaijan 0
Moldova 0 Netherlands 1
Montenegro 1 Switzerland 0
Serbia 1 Estonia 3
Wales 0 Bulgaria 1
Germany 3 Turkey 0
Greece v Latvia
Northern Ireland 0 Italy 0
Rep of Ireland 2 Russia 3
Slovenia 5 Faroe Islands 1
Portugal 3 Denmark 1
Spain 3 Lithuania 1
Nigeria yafunguliwa kwa muda
FIFA leo imetangaza kuwa imeondoa kwa muda amri ya kuifungia Nigeria kushiriki Mashindano ya Kimataifa baada ya kuridhika na mwelekeo thabiti wa kufuta kesi iliyokuwa Mahakamani kuwapinga Viongozi wa NFF, Chama cha Soka Nigeria, na pia kurudishwa madarakani kwa Katibu Mkuu wa NFF.
Taarifa rasmi iliyotolewa leo huko Zurich, Uswisi, Makao Makuu ya FIFA, ilisema: “Baada ya Mdai katika kesi iliyokuwa Mahakamani kutangaza waziwazi kuifuta kesi hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa NFF kurudishwa madarakani tangu Oktoba 5 na Ligi ya Nigeria kuachiwa NFF kuiendesha, kusimamishwa kwa Nigeria kunafutwa kwa muda hadi Oktoba 26 tutakapojua hatma ya kesi iliyopo Mahakamani itakayosikilizwa Oktoba 25. Endapo kesi hiyo itaendelea Mahakamani na ikiwa NFF itaendelea kuingiliwa, kusimamishwa kwa Nigeria kutaanza mara moja hadi matatizo yote yatakapokwisha.”
Jumapili Nigeria wanatakiwa wacheze mechi ya Kundi lao kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Conakry dhidi ya Guinea.
Mancini alikoka bifu na Fergie
Roberto Mancini wa Manchester City ameiponda Manchester United kwa kudai Chelsea na Arsenal ndio Timu zenye ufundi wa hali ya juu na hilo huenda likasababisha Sir Alex Ferguson wa Manchester United kukerwa na kuchochea zaidi uhasama kati ya Mahasimu hao wa Jijini Manchester.
Akiongea huko kwao Italia ambako alienda kumuuguza Baba yake, Mancini alisema: “Chelsea ndio Timu ngumu Ligi Kuu. Arsenal wako sawa nao kiufundi lakini wanazidiwa miguvu na Chelsea.”
Ingawa Man City iliifunga Chelsea 1-0 kwenye Ligi Kuu, Mancini anaamini Chelsea chini ya Mtaliana mwenzake Carlo Ancelotti itatwaa tena Ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara pili mfululizo.
Mancini aliongeza: “Baada ya mechi na Chelsea nilimwambia Carlo Ancelotti ‘Nimekufunga lakini mtashinda Ligi Kuu’! Nadhani Chelsea watachukua Ubingwa!”
Baada ya mechi 7, Chelsea wanaongoza Ligi wakifuatiwa na Man City, Man United na Arsenal na hii ni mara ya kwanza kwa Man City, kwenye hatua hii, kuwa mbele ya Man United katika Miaka 20.
Hata hivyo, Mancini anasema yeye na Wamiliki wa Klabu lengo lao ni kumaliza katika nafasi 4 za juu ili wacheze UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu wa 2011/12.
Mancini pia alisema amekuwa haongei na Mtaliana mwenzake Fabio Capello ambae ni Kocha wa England licha ya Man City kuwa na Wachezaji wengi Timu ya England.
No comments:
Post a Comment