Monday, 4 October 2010

Capello ataja Kikosi cha England
Kocha wa England Fabio Capello ametangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya Makundi ya EURO 2012 huko Wembley na Montenegro Oktoba 12 na miongoni mwa Wachezaji hao yupo Straika wa Bolton Simon Davies, Miaka 33, ambae hajawahi kuichezea England.
Mastraika wengine kwenye Kikosi hicho ni Wayne Rooney, Darren Bent na Peter Crouch.
Wachezaji wengine maarufu ambao wametajwa ni John Terry, Rio Ferdinand, Joe Cole, Aaron Lennon na Kipa Rob Green.
Chipukizi wa Arsenal Jack Wilshere nae yumo kundini.
Kwenye Kundi lao, England tayari wameshacheza mechi mbili na kuzishinda Bulgaria na Uswisi.
Kikosi kamili cha England ni:
Ben Foster (Birmingham City), Robert Green (West Ham United), Joe Hart (Manchester City) , Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Rio Ferdinand (Manchester United), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Stephen Warnock (Aston Villa), Gareth Barry (Manchester City), Joe Cole (Liverpool), Steven Gerrard (Liverpool), Tom Huddlestone (Tottenham Hotspur), Adam Johnson (Manchester City), Aaron Lennon (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Ashley Young (Aston Villa), Darren Bent (Sunderland), Peter Crouch (Tottenham Hotspur), Kevin Davies (Bolton Wanderers), Wayne Rooney (Manchester United)
De Jong atemwa Holland kwa uchezaji rafu!
Kiungo wa Manchester City Nigel de Jong ametupwa nje ya Timu ya Uholanzi kwa mechi za EURO 2012 dhidi ya Moldova na Sweden kwa kile Kocha wa Timu hiyo ya Taifa, Bert Van Marwijk, kukiita uchezaji wa mabavu kupindukia.
Jumapili kwenye mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester City na Newcastle De Jong alimvunja mguu Hatem Ben Arfa na Kocha Marwijk ametamka: “Ni mbaya na ilikuwa si lazima! Nina matatizo na uchezaji wa De Jong anaecheza kwa nguvu kupindukia.”
Hiyo si mara ya kwanza kwa De Jong kumvunja mtu mguu kwani Mwezi Machi alimvunja Mchezaji wa USA Stuart Holden, ambae pia huchezea Bolton.
Lakini Dunia inamkumbuka vizuri De Jong kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Spain ilipocheza na Holland huko Afrika Kusini na De Jong kumshindilia Xabi Alonso wa Spain guu la kifuani lakini akaepuka kutolewa.

No comments:

Powered By Blogger