Monday, 4 October 2010

Ben Arfa avunjwa mguu
Kiungo wa Newcastle Hatem Ben Arfa amevunjika mguu katika mechi ya Ligi Kuu waliyofungwa 2-1 na Manchester City Jumapili.
Ben Arfa, Miaka 23, aliumizwa na Nigel De Jong dakika ya 4 tu ya mchezo na kukimbizwa hospitalini.
Bosi wa Necastle, Chris Hughton, amethibitisha kwa kusema: “Aliumizwa katika rafu isiyostahili.”
Ben Arfa yupo Newcastle kwa mkopo akitokea Marseille ya Ufaransa na hiyo ilikuwa mechi yake ya tatu.
Hodgson: ‘Huu ni mwanzo usiokubalika!’
Bosi wa Liverpool, Roy Hodgson, amesema matokeo wanayopata Liverpool kwa sasa ni mwanzo mbaya wa Msimu na hayakubaliki.
Jumapili, Liverpool wakiwa nyumbani Anfield, walipigwa 2-1 na Blackpool kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyowafanya wawe nafasi ya tatu toka mkiani kwenye eneo la kuporomoka Daraja.
Hodgson ametamka: “Ni mwanzo mbaya wa Msimu. Hatufurahii na lazima tubadilike. Tuna kazi ngumu.”
Real Madrid 6 Deportivo 1
Huko kwenye La Liga Nchini Spain Jumapili Vigogo Real Madrid wameinyuka Deportivo la Coruna mabao 6-1 na kushika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi.
Awali, FC Barcelona walitoka sare 1-1 na Mallorca.
Baada ya mechi 6, Valencia ndie kinara akiwa na pointi 16, Viillareal ni wa pili akiwa na pointi 15, Real Madrid pointi 14 na Barcelona pointi 13.
Katika mechi hiyo ya Real, Wafungaji wao walikuwa Cristiano Ronaldo mabao mawili na wengine ni Mesut Oezil, Angel Di Maria na Gonzalo Higuain.
Bao jingine lilifungwa na Ze Castro wa Deportivo aliejifunga mwenyewe.

No comments:

Powered By Blogger